FAHAD AHMAD
Tuesday, January 28, 2014
UISLAMU NA SUALA LA HIJABU-I
JIULIZE:1·NINI MTIZAMO WA UISLAMU KATIKA SUALA LA HIJABU KWA MWANAMKE NA HAKI YAKE YA KUSOMA NA KUFANYA KAZI.
2·JE NI KWELI KUWA HIJABU HAIENDI SAMBAMBA NA MAISHA YA LEO? (IMEPITWA NA WAKATI).
Kwanza kabisa ni vema tukaelewa tunapozungumzia Hijabu tunazungumzia nini. Tunapoizungumzia Hijabu tunaikusuduia Hijabu kama ilivyo ndani ya Qur - ani Tukufu. Neno Hijabu limetumika ndani ya Qur - ani zaidi ya mara nane. Miongoni mwa aya zilizoitaja Hijabu ndani ya Qur - ani ni hizi zifuatazo:-
".. NANYI MNAPOWAULIZA (wakeze Mtume) WAULIZENI NYUMA YA PAZIA (Hijabu) ..." (33:53)
Hii ndio Hijaabu kwa lugha ya Qur - ani:-
"(NA WAKASEMA: "NYOYO ZETU ZI KATIKA VIFUNIKO KWA YALE UNAYOTUITIA; NA KATIKA MASIKIO YETU MUNA UZITO; NA BAINA YETU NA BAINA YAKO KUNA PAZIA. (Hijaabu) ???" (41:5)
Ione Hijaabu kupitia Qur - ani:-
"BASI AKASEMA ; NAVIPENDA VITU VIZURI KWA KUMKUMBUKA MOLA WANGU. KISHA (mafarasi) WAKAFICHIKANA NYUMA YA KIZIUIZI (Hijaabu, kwa kutiwa zizini mwao)" (38:32)
Ijue Hijaabu kupitia Qur-ani-
"NA AKAWEKA PAZIA (Hijaabu) KUJIJINGA NAO??.." 19:170.
Ielewe Hijaabu kupitia Qur-ani- "NA UNAPOSOMA QUR-ANI (inakuwa kama kwamba) TUMETIA BAINA YAKO NA BAINA YA WALE WASIOAMINI AKHERA PAZIA LILILOFUNIKWA (sana hata hawafahamu kinachosemwa)" (17:45)
Hizi ndizo baadhi ya aya za Qur-ani Tukufu ambazo ndani yake limetajwa na kutumika neno "Hijaabu". Kupitia aya hizi tunaweza kusema kuwa Hijaabu ya Kiislamu ni:-
a)Sitara ya kutokuchangayika pamoja wanume na wanawake.
b)Sitara ya kutokusikia sauti ya mwanamke kwa mwanamume.
c) Sitara ya mwili (mavazi) yaani kutoonekana mwili wa mwanamke ila na maharimu zake tu.
Hii ndio eleweko la Hijaabu kwa mtazamo wa kiislamu, kama tutakavyolithibitisha hilo na kulijengea hoja kupitia Qur-ani yenyewe. Hijaabu hailengi ila kuwa ni chombo cha kujenga na kuratibisha uhusiano mwema uliopo baina ya jinsia mbili zihitajianazo na kutegemeana, mwanamume na mwanamke. Huu ni utaratibu na nidhamu ya lazima inayozisaidia jinsia mbili hizi kuistawisha dunia na kuyafurahia maisha katika misingi waliyowekewa na Mola Muumba wao. Kila mmoja, mwanamume na mwanamke ameamrishwa na kukalifishwa kuishi kwa kuufuata utaratibu na nidhamu hii. Hii ni kwa ajili ya kuidhibiti na kuitawala nguvu ya kimaumbile iliyopo baina ya jinsia mbili hizi. Nguvu ambayo ina athari kubwa katika kuvuruga na kuharibu mwenendo na silka nzima ya mwanadamu. Mvuto na matamanio ya kijinsia alio nayo mwanamume, yanapatikana pia kwa mwanamke. Kila mmoja kwa mwenzie ni mfano wa sumaku inayokivuta chuma na hatimaye kukinasa na kushikamana nacho. Haya ndio maumbile yaliyokamilika na chanzo/sababu yake ya msingi ni "Homonsi" alizoumbiwa kila mmoja wao. Ni kwa kulijua na kuzingatia tabia hii ya maumbile ya mwanadamu ndio tunaikuta Hijaabu hata katika vilabu vya Mwenyezi Mungu Mtukufu vilivyoitangulia Qur-ani.
Hijaabu ya Kiislamu haikomelei tu katika kusitiri na kuhifadhi mapambo (sehemu zenye kuamsha na kuchochea fitna kati ya mwanamume na mwanamke), na kuinamisha macho tu bali Hijaabu ni pamoja na:-
1·Kutokukaa faraghani mwanamume na mwanamke. Haya ndiyo maelekezo na mafundisho ya Bwana Mtume- Rehema na Amani zimshukie - kupitia kauli yake:-"Asikae, asikae, rafaghani mmoja wenu na mwanamke ila (awe pamoja na mwanamke huyo) maharimu (yake, baba, kaka, babu n.k). Bukhariy na Muslim.
2·Kutogusana mwili na mwanamume na mwanamke. Haya ndio mafundisho ya Uislamu kupitia kauli ya Mtume wa Uislamu- Rehema na Amani zimshukie:- "Mmoja wenu kuchomwa kichwani kwake na sindano ya chuma na bora kwake kuliko kumgusa mwanamke asiye halali yake" Twabaraany. Amesema mkewe Bwana Mtume , Bi Aysha- Allah amuwiye radhi: "Wallah! Mkono wa Mtume wa Mwenyezi Mungu Haukupata kabisa kumgusa mwanamke (asiye halali yake), ila alikuwa akipeana nao ahadi kwa maneno (kwa kuzungumza) tu"
3·Mwanamke kutokulegeza sauti yake mbele ya mwanamume. Tusome: ENYI WAKE WA MTUME, NINYI SI KAMA YOYOTE TU KATIKA WANAWAKE WENGINE (ninyi wakeze Mtume). KAMA MNATAKA (kufanya jambo la) KUMCHA ALLAH, BASI MSILEGEZE SAUTI (zenu mnaposema na wanaume) ILI ASITAMANI MTU MWENYE UGONJWA MOYONI MWAKE (kufanya mabaya na nyie) NA SEMENI MANENO MAZURI " (33:32). Semezo (kihitwaabu) la aya hii linaelekezwa moja kwa moja kwa wakeze Bwana Mtume lakini amri hii inawahusu na kuwaenea wanawake wote wa Kiislamu.
4·Kuzuia picha, magazeti, majarida, vipeperushi, nakala na matangazo ambayo kwa namna moja au nyingine huchochea na kuamsha tmaa na matamanio ya kimwili.
5·Mwanamke kujitia manukato na kupita mbele ya wanaume . Bwana Mtume - Rehema na Amani zimshukie - anatahadharisha juu ya hili kwa kutuambia "Mwanamke yeyote atakayejitia manukato na kupita mbele ya wanamume ili waipate harufu ya (manukato) yake, basi mwanamke huyo ni mzinifu (anapata dhambi za kuzini kwa sababu ya kushawishi kwake zinaa) na kila jicho (limtazamalo) pia ni zinifu" Abuu Daawoud, Tirmidhiy, Nasaai, Ibn Khuzaymah na Ibn Hibban.
Haya ni baadhi tu ya maeneo yanayoguswa moja kwa moja na Hijaabu ya Kiislamu. Msingi na asili ya suala la Hijaabu ni kauli tukufu ya Mwenyezi Mungu Mtukufu ndani ya Qur-ani Tukufu isemayo "NA WAAMBIE WAISLAMU WANAWAKE WAINAMISHE MACHO YAO, NA WAZILINDE TUPU ZAO WALA WASIDHIHIRISHE VIUNGO VYAO ISIPOKUWA VINAVYODHIHIRIKA (nao ni uso na vitanga vya mikono). NA WAANGUSHE SHUNGI ZAO MPAKA VIFUANI MWAO, NA WASIONYESHE MAPAMBO YAO ILA KWA WAUME ZAO, AU BABA ZAO, AU BABA ZA WAUME ZAO (wakwe zao) AU WATOTO WAO, AU WATOTO WA WAUME ZAO, AU KAKA ZAO, AU WANA WA KAKA ZAO, AU WANA WA DADA ZAO, AU WANAWAKE WENZIWAO, AU WALE ILIYOWAMILIKI MIKONO YAO YA KIUME (watumwa wao) AU WAFUASI WANAUME WASIO NA MATAMANIO ( kwa wanawake) AU WATOTO AMBAO HAWAJAJUA MAMBO YANAYOHUSU UKE, WALA WASIPIGE MIGUU YAO ILA YAJULIKANE WANAYOYAFISHIA KATIKA MAPAMBO YAO NA TUBIENI NYOTE KWA ALLAH ENYI WAISLAMU ILI MPATA KUFAULU" (24:31).
Alisema Bwana Mtume - Rehema na Amani zimshukie - wakati Asmaa Bint Abuu Bakri - Allah awawiye radhi wote - alipoingia kwa Mtume akiwa amevaa nguo nyepesi: "Ewe Asmaa, hakika mwanamke anapofikilia umri wa kupata hedhi (anapovunja ungo) haifai kuonekanwa (mwili) wake ila hiki na hiki. Na (Mtume) akaashiria uso na vitanga vyake" Abuu Daawoud.
Miongoni mwa sharti za Hijaabu ya vazi la mwanamke wa Kiislamu ni kwamba:-
a)Isiwe nguo yenyewe ni pambo linaloweza kumvutia mtazamaji. Hilo ndilo eleweko na fahamisho la kauli ya Allah isemayo" "WALA WASIDHIHIRISHE MAPAMBO YAO??." (24:31) Na kauli isemayo, "NA KAENI MAJUMBANI MWENU, WALA MSIONYESHE MAPAMBO YENU KAMA WALIVYOKUWA WAKIONYESHA MAPAMBO YAO WANAWAKE WA ZAMA ZA UJAHILI (Ujinga ukafri)??.' (33:33).
b)Iwe nzito isiwe nyepesi ionyeshayo rangi ya mwili. Hii ni kutokana na kauli ya Mtume isemayo:" Watakuwepo mwisho wa umati wangu wanawake watakaovaa (lakini) wako uchi. Vichwani mwao kuna nundu (kutokana na mitindo ya nywele) kama nundu za ngamia. Walaanini kwa kuwa wao wamelaaniwa??" Ahmad.
c)Isiwe yenye kubana sana kiasi cha kuonyesha ramani/finyango la mwili.
d)Isiwe imetiwa manukato au kufukizwa kwa udi, Haya ni kwa mujibu wa kauli ya Bwana Mtume - Rehema na Amani zimshukie aliposema" Mwanamke yeyote atakayejitia manukato, kisha akapita mbele ya wanaume ili waipate harufu yake, basi yeye ni mzinifu",
e)Isifanane na nguo za wanaume, hivyo ndivyo tunavyofahamu kutokana na kauli ya Bwana Mtume - Rehama na Amani zimshukie - isemayo: "Si katika sisi mwanamke mwenye kujishabihisha na wanaume wala mwanaume mwenye kujishabihisha na wanawake. Twabaraaniy na Ahmad.
HAKI YA JIRANI
Tuanze na kujiuliza, jirani ni nani? Jirani tunayemkusudia hapa ni yule mtu aliye karibu yako kimakazi, yaani nyumba zenu zinakurubiana. Mtu mwenye wasifu huu ana haki kubwa juu yako, ewe muislamu. Itakaposadifu kwamba jirani yako ni ndugu yako wa nasabu na akawa ni muislamu mwenzako. Basi jirani huyu atakuwa ana haki tatu kwako; haki ya ujirani, haki ya udugu na haki ya Uislamu. Na akiwa jirani yako ni muislamu lakini si nduguyo wa nasabu, huyu atakuwa nazo kwako haki mbili; haki ya ujirani na haki ya Uislamu. Na iwapo jirani yako huyu si muislamu na hapana udugu baina yenu, jirani huyu atamiliki kwako haki moja tu nayo ni haki ya ujirani. Hivi ndivyo anavyotufundisha Mtume wa Allah-Rehema na Amani zimshukie: “Majirani ni watatu; jirani mwenye haki moja naye ndiye mwenye haki ndogo kuliko wote. Na jirani mwenye haki mbili na jirani mwenye haki tatu. Ama yule ambaye mwenye haki moja ni jirani mushriki (kafiri), na ama ambaye mwenye haki mbili ni jirani muislamu (ana) haki ya Uislamu na haki ya ujirani. Na ama yule mwenye haki tatu ni jirani muislamu aliye ndugu, (ana) haki ya Uislamu, haki ya ujirani na haki udugu”. Al-Bazzaar & Abuu Nuaim.
Muislamu anakiri, anaikubali na kuichunga haki ya jirani akiamini kuwa kufanya hivyo ni kuitekeleza amri ya Mola wake: “MWABUDUNI ALLAH WALA MSIMSHIRIKISHE NA CHO CHOTE NA WAFANYIENI IHSANI WAZAZI WAWILI NA JAMAA NA MAYATIMA NA MASKINI NA JIRANI WALIO KARIBU NA JIRANI WALIO MBALI--- [ 4 : 36] Naye Mtume wa Allah–Rehema na Amani zimshukie-kama mfasiri mkuu wa Qur–ani, anauelezea uzito wa haki hii ya jirani iliyotajwa ndani ya Qur-ani anasema: “Hakuacha Jibril kuniusia juu ya jirani mpaka nikadhani kwamba atampa na haki ya kurithi”. Bukhaariy & Muslim.
Miongoni mwa haki za jirani kama zilivyoelezwa na Uislamu ni kumtendea wema kiasi cha uwezo wa mtu. Mtendee wema jirani yako kwa mali yako, cheo chako na kila chako chenye kuweza kumnufaisha kwa namna moja au nyingine. Hivi ndivyo anavyo tufundisha. Mtume wa Allah–Rehema na Amani zimshukie– kutokana na kauli yake: “Jirani bora mbele ya Allah ni yule aliye mwema kwa jirani yake”. Tirmidhiy.
Na akasema tena Bwana Mtume: “Mwenye kumuamini Allah na siku ya mwisho basi na amtendee wema jirani yake”. Muslim.
Kauli hii ya Mtume wa Allah kama inafahamisha jambo, basi jambo hilo si jingine bali ni kuwa ukitaka kumjua muumini wa kweli basi muangalie anavyoishi na jirani yake. Imepokelewa kutoka kwa Muawiyah Ibn Jundub-Allah amuwiye radhi–kwamba alimuuliza Mtume wa Allah–Rehema na Amani zimshukie: “Ewe Mtume wa Allah, ni ipi haki ya jirani kwa jirani yake? Mtume akamjibu:-
Akiugua mkague (mtake hali),
Akifa msindikize (nenda kamzike),
Akikuomba mkopo, mkopeshe,
Akienda utupu (hana nguo), msitiri ( mvike ),
Akipatwa na kheri, mpongeze,
Akipatwa na msiba, muizi (mfanyie ta’azia),
Wala usinyanyue nyumba yako zaidi kuliko nyumba yake ukamzibia hewa/upepo,
Na wala usimuudhi kwa harufu ya chungu chako ila umchotee kidogo”. Twabaraaniy
Kumtendea wema jirani alikokueleza Bwana Mtume katika hadithi tulizozitaja ni pamoja na kumpelekea zawadi katika furaha mbali mbali anazozipata. Mithili ya kufaulu katika mtihani, kupata cheo, kuzaliwa mtoto, kuoa/kuozesha, kujenga nyumba na kadhalika. Falsafa na siri ya kupeana zawadi ni kujenga mapenzi na kuondosha chuki na uadui kama anavyolibainisha hilo Mtume wa Allah–Rehema na Amani zimshukie: “Peaneni zawadi mtapendana, na peaneni mikono itakuondokeeni chuki baina yenu”. Ibn Asaakir.
Na katika jumla ya haki za jirani ni kutokumuudhi kwa kauli au matendo. Siku moja Mtume wa Allah–Rehema na Amani zimshukie– alisema: “Wallahi hawi muumini, Wallahi hawi muumini, Wallahi hawi muumini. Maswahaba wakamuuliza: Ni nani huyo ewe Mtume wa Allah? Akajibu: Huyo ni yule ambaye jirani yakke hasalimiki na shari/uovu wake”. Bukhaariy
Mtu mmoja alimuendea Mtume wa Allah na kumuambia: “Hakika mwanamke fulani anatajwa sana kwa wingi wa swala zake, kutoa kwake sadaka kwa wingi na wingi wa kufunga kwake. Isipokuwa kwamba yeye anamuudhi jirani yake kwa ulimi wake. Mtume akasema: “(Pamoja na ibada zake zote hizo, mwanamke) huyo ataingia motoni”. Ahmad, Al-Bazzaar, Ibn Hibbaan & Al-haakim.
Kauli hii ya Mtume wa Allah inaonyesha uzito wa dhambi ya kumuudhi jirani na kwamba ibada ya mtu anayemfanyia maudhi jirani yake haitamsaidia kuingia peponi jirani huyo mbaya. Na kinyume chake, kutokumuudhi jirani ni sababu tosha inayoweza kumuingiza mtu peponi, kwani kukaa kwa wema na jirani bila ya kumuudhi kwa maneno au matendo ni kielelezo cha wema wa mja. Imepokelewa kwamba mtu mmoja alimwambia Mtume wa Allah– Rehema na Amani zimshukie–nijulishe amali ambayo nitakapoitenda nitaingia peponi. Mtume akamjibu: “Kuwa mwema”. Akasema mtu yule: Ewe Mtume wa Allah, nitajuaje kwamba mimi ni mwema?
Mtume akamwambia: Waulize jirani zako, wakikuambia kwamba wewe ni mtu mwema basi fahamu kwamba wewe ni mwema (kweli). Na wakikuambia kwamba wewe ni mtu mbaya (muovu), basi fahamu kwamba wewe ni mbaya (kweli )”. Al-Baihaqiy
Huyu ndiye jirani na haki yake katika Uislamu, lakini watu wengi miongoni mwetu hawaijali haki hii ya ujirani. Kutokuitambua haki hii ya ujirani ndio imekuwa sababu kuu ya magomvi uadui na mizozo mitaani mwetu. Utawaona majirani daima wakigombana kwa mambo ya kipuuzi kabisa kiasi cha kuwafanya wasijuliane hali na kutokushirikiana katika furaha wala huzuni. Huu si Uislamu aliokuja nao Bwana Mtume kutoka kwa Allah, muislamu wa kweli haishi hivyo na jirani yake hata kama si muislamu mwenziwe(kafiri )

KUJIZUIA NA HARAMU NA MAMBO MACHAFU
Chimbuko na chemchem ya somo letu hili linalobeba anuani ya kujizuia na haramu/mambo machafu ni kauli yake MwenyeziMungu aliposema :
“NA WAJIZUILIYE NA MACHAFU WALE WASIOPATA CHA KUOLEA MPAKA AWATAJIRISHE KATIKA FADHILA ZAKE …..” [24:33]
Kujizuia na haramu/mambo machafu ni nguvu na uwezo uliomo ndani ya nafsi ya binadamu wa kuyadhibiti na kuyashinda matashi na matamanio ya nafsi yake yasimpondoe na njia ya MwenyeziMungu, ambayo ghalibu/mara nyingi ndio kazi ya nafsi kama tunavyosoma :
“NAMI SIJITAKASI NAFSI YANGU; KWA HAKIKA (kila) NAFSI NI YENYE KUAMRISHA SANA MAOVU, ISIPOKUWA ILE AMBAYO MOLA AMEIREHEMU….” [12:53]
Kuizuia nafsi na mambo yaliyoharamishwa ambayo mengine hujidhihirisha katika sura ya mvuto na ladha kiasi cha kuichukua mateka nafsi ya mwanadamu, ni miongoni mwa mambo na sifa tukufu anazotakiwa kupambika nazo mwanadamu ili apate kuushinda ule unyama alioumbiwa na kuwa mtu mkamilifu wa utu na ubinadamu. Mwanadamu akiweza kufika hapo kwa kuyashinda matashi na matamanio ya nafsi yake basi atakuwa amejihakikishia kufaulu leo ulimwenguni na kesho akhera. Haya yamethibitishwa na maneno matukufu ya MwenyeziMungu :
“NA KWA NAFSI NA ALIYEITENGENEZA. KISHA AKAIFAHAMISHA UOVU WAKE NA WEMA WAKE. BILA SHAKA AMEFAULU ALIYEITAKASA (nafsi yake). NA BILA SHAKA AMEJIHASIRI ALIYEUZA (nafsi yake) [91:7-10]
Kutokana na aya hizi tunatambua kuwa kumbe nafsi ya mwanadamu tayari imekwishapewa uwezo na ujuzi wa kujua jema na baya na kisha ikaachiwa uhuru wa kuchagua kufuata jema au baya/ovu ili ikalipwe kesho akhera kwa mujibu wa uchaguzi ilioufanya hapa duniani. Qur-ani inatuambia :
“HAKIKA SISI TUMEMUONGOZA (tumembainishia) NJIA (zote mbili: kuwa hii ndiyo ya kheri na hii ndiyo ya shari) BASI (mwenyewe tena) ATAKUWA MWENYE SHUKRANI AU AWE MWENYE KUKUFURU (kukanusha)” [76:3]
Uwezo wa kujizuia na haramu/ mambo machafu huzaa tabia njema na nzuri, uwezo huu humfanya mwanadamu awe na subira kwa maana ya subira ya kweli. Aweze kusubiri kuyashinda maovu na kuendelea kusubiri katika kutenda mema ambayo mara nyingi nafsi huyaona kuwa ni magumu na mazito. Humpa mwanadamu kukinai na kutosheka na kile alichokadiriwa na kupewa na Mola wake, jambo ambalo ni utajiri mkubwa kama alivyosema Bwana Mtume –Rehma na amani zimshukie –
“Utajiri si (mtu) kuwa na mali nyingi lakini utajiri ni utajiri wa nafsi (ya mtu kutosheka)” Ahmad, Muslim, na Tirmidhi.
Kujizuiya na haramu humfinyanga mwanadamu kuwa mkarimu na mpaji. Kwa ujumla tunaweza kusema nguvu na uwezo huu wa kuidhibiti nafsi isifuate matashi na matamanio yake ni KHAZINA ya asokuwa na mali na ni taji la asokuwa na utukufu.
Hebu na tujiulize basi ni nini sababu ya utukufu huu au mwanadamu afanye nini hata aweze kuifikia daraja hii tukufu ambapo ataweza kuwa juu ya nafsi yake akaweza kuitawala na sio nafsi kumkalia mbele na kumburuzia ? Mwanadamu hawezi kukifikia kilele hiki ila kwa kuachana na :
Tamaa mbaya. Bwana Mtume –Rehma na amani zimshukie – anatuasa : “Jilindeni kwa Allah kutokana na tamaa yenye kupelekea katika chuki/ghadhabu na (kutokana) na tamaa iongozayo kwenye kisichotumainiwa na (kutokana) na kutamani pasipo na matumaini”. Ahmad,Al-twabraaniy na Al-haakim.
Pupa katika kuchuma mali : Hili ndio mama wa maovu yote, kwa sababu mwanadamu anapokuwa lengo lake ni kujikusanyia na hatimaye kujilimbikizia mali kwa kuichelea umasikini, basi sera zake huwa ni kupata tu bila kuzingatia anapata kwa njia gani, ya halali au ya haramu. Katika hali hii mwanadamu huyu yuko tayari kukabiliana na kikwazo chochote kinachoweza kumzuia asifikie lengo lake; hata ikibidi kuitoa roho ya mwanadamu mwenziwe ndipo apate, basi yuko tayari kufanya hivyo kwa gharama yeyote ile. Mtume wa MwenyeziMungu – Rehma na amani zimshukie – anatuhadharisha : “Hakika kila umati una fitna yake na fitna ya umati wangu ni mali” Al-tirmidhi, Ibn Hibbaan, na Al-Haakim.
Kuridhia na kichache unachokipata. Amesema Bwana Mtume – Rehma na amani zimshukie – “Bila ya shaka amefaulu aliyejinyenyekesha kwa Mola wake na akaruzukiwa chenye kumtosha na MwenyeziMungu akamkinaisha na alichompa” Ahmad, Muslim, Al-tirmidhi, na Ibn Maajah.
Mwanadamu hawezi kuifikia daraja ya kujizuia na haramu/mambo machafu kwa ukamilifu, mpaka pale atakapoweza kuukemea na kuuzuia ulimi wake, macho, masikio, tumbo na baki ya viiungo vyake vingine vya mwili. Asiunyooshe mkono wake katika kutoa au kupokea rushwa, asiutumie mkono wake kumdhuru mtu bila ya haki, asiutumie ulimi wake kutukana, kufitinisha, kusengenya, kusema uongo, kutoa ushahidi wa uongo na kama hayo. Ayazuiliye masikio yake kusikiliza maneno machafu ya kipuuzi na kila kilichoharimishwa kukisikiliza. Macho yake yasiwaangalie wanawake/wanaume wasio halali yake, asivikodolee macho ya tamaa vilivyomo mikononi mwa watu, asiwatizame watu kwa jicho la dharau. Asiliruhusu tumbo lake kula riba, mali ya yatima na chochote kile kilichoharimishwa. Asiitumie tupu (uchi) yake mahala pasipo halali yake. Ili mradi anatakiwa akizuie kila kiungo chake na kila lililoharamishwa na kukatazwa huku akiitafakari kauli ya Mola wake :
“HAKIKA MASIKIO NA MACHO NA MOYO; HIVYO VYOTE VITAULIZWA” [17:36]
Mtume wa MwenyeziMungu – Rehma na amani zimshukie – anatuambia “Ukiwa nayo mambo matatu basi hakikudhuru kilichokufutu/kilichokupita katika dunia; ukweli wa mazungumzo, kuhifadhi amana na kujizuia na tamaa”
TUJIFUNZE NA TUKUBALI KUWA : Dini ni tabia njema, ndio maana Bwana Mtume anatuambia sababu ya kuletwa kwake kwa kusema : “Hakika si vinginevyo, sikutumilizwa ila kuja kukamilisha tabia njema” Ibn Sa’d, Al-Bukhariy, Al-Haakim, na Al-Bayhaqiy.
Sote tunakubali kuwa KUKAMILISHA sio kuasisi wala kuanzisha, kwa msingi huu tunaelewa kuwa Bwana Mtume hakuja kuasisi kitu kipya bali amekuja kumalizia kazi iliyoasisiwa na nduguze mitume waliotangulia kabla yake.
Miongoni mwa tabia njema unazopaswa kupambika nazo ni hii ya kujizuia na haramu/mambo machafu. Anza sasa kusema na kuikemea nafsi yako na shetani, huku ukitambua kuwa wawili hao ndio maadui zako wakubwa.
“KWA YAKINI SHETANI NI ADUI YENU, BASI MFANYENI ADUI (yenu: kwa hiyo msimtii) KWANI ANALIITA KUNDI LAKE LIWE KATIKA WATU WA MOTONI” [35:6]

KUTEKELEZA AHADI
i/ Kutekeleza ahadi ni miongoni mwa tabia njema/tukufu anazotakiwa ajipambe nazo muislamu wa kweli. Muislamu anapotoa ahadi, basi atambue kwamba amelazimishwa na sheria kuitekeleza ahadi muda wa kuwa si katika kumuasi Mola Mtukufu. Mwenyezi Mungu atuambia:-"NA TIMIZENI AHADI. KWA HAKIKA AHADI ITAULIZWA (siku ya kiama) (17:34)Kukhalifu au kutokutimiza ahadi ni katika jumla ya alama za unafiki wa mtu kama anavyotubainishia hilo Bwana mtume: "Alama za mnafiki ni tatu:anapozungumza husema uwongo, na akiahidi hukhalifu (hatekelezi ahadi) na akiaminiwa hufanya khiyana". Bukhaariy na muslimu.
Tabia ya kutekeleza ahadi humfanya mtu aaminiwe na watu, atajwe vema katika uhai na baada ya kufa kwake kama Qur-ani inavyotuambia:
"NA MTAJE KATIKA KITABU (hiki) ISMAIL. BILA SHAKA YEYE ALIKUWA MKWELI WA AHADI, NA ALIKUWA MTUME, NABII". (19:54)
Mwenyezi Mungu amuambia Nabii Muhammad amtaje na kumkumbuka Mtume wake Ismail ndani ya Qur-ani baada ya kupita chungu ya miaka kwa sababu ya kupambika kwake na tabia tukufu ya kutekeleza ahadi. Anayetoa ahadi na kutimiza basi atambue kwamba amepambika na sifa miongoni mwa sifa za mitume. Sifa hii kutekeleza ahadi huambatana na sifa mbili kuu; kusema ukweli na kutokukhini amana. Basi ukimuona mtu atekeleza ahadi basi mshuhudie pia kuwa ni mkweli asiye na khiyana.
ii/ UKWELI
Ukweli ni mtu kulieleza jambo kama kilivyo bila yakupunguza au kuzidisha chochote.
Muislamu huwa ni mkweli apendaye kusema ukweli na kujitazamisha na tabia ya ukweli hii ni kwa sababu anatambua ukweli humuongezea katika wema, wema ambao humuongoza (kumpeleka) peponi na pepo ndio lengo kuu la muislamu. Muislamu hauangalii ukweli kama ni tabia njema anayopaswa kujipamba nayo tu bali huenda mbali zaidi ya hapo. Huuona ukweli kuwa ni miongoni mwa mambo yanayoikamilisha imani na uislamu wake: Mwenyezi Mungu anatuagiza:-
"ENYI MLIOAMINI: MCHENI ALLAH NA KUWENI PAMOJA NA WAKWELI" (9:119)
Ukweli umejengeka juu ya sababu tatu, ambazo ni:-
Akili – akili timamu ndio humfanya mtu anayetambua manufaa ya ukweli na madhara ya uwongo.
Murua – mtu mwenye murua, murua wake haumruhusu na kumuachia kusema uwongo bali humlazimisha ajipambe na tabia ya ukweli
Dini – Dini pia humfinyanga mtu ksema ukweli kwa kuamini kuwa dini inamuamrisha kusema ukweli na inamkataza kusema uwongo.
Ukweli pia ni miongoni mwa sifa njema walizopambika nazo Mitume wa Mwenyezi Mungu. Qur-ani yatuambia:- "NA MTAJE IDRIS KATIKA KITABU (hiki). BILA SHAKA YEYE ALIKUWA MKWELI SANA NA NABII". (19:56)
Tabia ya ukweli huzaa matunda mema na mazuri ambayo huvunwa na watu wakweli. Miongoni mwa matunda hayo ni:-
Utulivu wa nafsi – Mwenye kupambika na tabia ya ukweli huwa na utulivu wa nafsi kwa mujibu wa kauli ya Mtume: "Ukweli ni utulivu" – At-tirmidhiy
Baraka katika chumo na ziada ya kheri – Bwana Mtume amesema: "Wauzianaji(Muuzaji na mnunuzi) wana khiyari (ya kupitisha au kuvunja biashara) muda wa kuwa hawajatengana, wakiwa wakweli na wakabainisha (aibu za kinachouzwa) watabarikiwa katika biashara yao, na wakificha (aibu) na wakasema uongo itafutwa baraka ya biashara yao" Al-bukhaariy
Kufuzu kwa kupata daraja ya mashahidi, hili linathibitishwa na kauli ya Mtume aliposema: "Mtu atakayemuomba Mwenyezi Mungu kufa shahidi kwa ukweli, Mwenyezi Mungu atamfikisha daraja ya mashahidi hata akifia kitandani". Muslim
Kuepuka balaa, inasimuliwa kwamba mtu mmoja aliyekuwa anakimbizwa alikimbilia kwa mtu mwema mmoja akamuomba amfiche hasikamatwe. Yule mtu mwema akamwambia; "Lala hapa", akamfunika na rundo la makuti. Wale waliokuwa wanamkimbiza wakapita pale kwa yule mtu mwema wakamuuliza :"Umemuona mtu akipita hapa anakimbia?" Akawajibu: "Huyo hapo chini ya makuti". Wale watu wakamuona nawafanyia maskhara wakampuuza wakaenda zao. Yule mtu aliyekuwa akikimbizwa akaokoka kwa bababu ya ukweli wa mtu mwema yule.
Kuchuma mapenzi ya Mola na watu. Mtu mkweli hupendeza mbele ya Mwenyezi Mungu na watu na watu wema humpenda.
Friday, January 17, 2014
Allaah Akimtakia Kheri Mja Humpa Mtihani Duniani
عَنْ
أَنَسٍ (رضي الله عنه) قَال: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ (صلى الله عليه و آله
وسلم): ((إِذَا أَرَادَ اللَّهُ بِعَبْدِهِ الْخَيْرَا عَجَّلَ لَهُ
الْعُقُوبَةَ فِي الدُّنْيَا وَإِذَا أَرَادَ اللَّهُ بِعَبْدِهِ الشَّرَّ
أَمْسَكَ عَنْهُ بِذَنْبِهِ حَتَّى يُوَافِيَ بِهِ يَوْمَ الْقِيَامَةِ))
وَ قال النَّبِيِّ (صلى الله عليه و آله وسلم): ((إِنَّ عِظَمَ الْجَزَاءِ
مَعَ عِظَمِ الْبلآءِ وَإِنَّ اللَّهَ إِذَا أَحَبَّ قَوْمًا ابْتَلاَهُمْ
فَمَنْ رَضِيَ فَلَهُ الرِّضَا وَمَنْ سَخِطَ فَلَهُ السَّخَطُ)) رواه
الترمذي وقال حديث حسن
Imepokelewa kutoka kwa Anas (رضي الله عنه) amesema: Mtume wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Allaah
Anapompendelea mja Wake kheri, Humharakishia adhabu duniani. Na Allaah
Anapomtakia mja Wake shari, Humzuilia dhambi zake mpaka Amlipe Siku ya
Qiyaamah)). Na amesema Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم): ((Hakika malipo makubwa kabisa yapo pamoja na mtihani mkubwa, na hakika Allaah Anapowapenda watu Huwapa mtihani. Basi atakayeridhika, atapata Radhi [za Allaah] na atakayechukia, atapata hasira. [za Allaah]))[1]
Mafunzo Na Hidaaya:
- Allaah (سبحانه وتعالى) Huwa pamoja na anayesibiwa na mitihani akasubiri, na juu ya hivyo, ni alama ya mapenzi ya Allaah (سبحانه وتعالى). [Aal-‘Imraan 3: 146, Al-Baqarah 2: 153, Al-Anfaal 8: 46].
- Alama za kufutiwa dhambi Muislamu anapokuwa na subra katika mitihani.
- Watu hupewa mitihani kulingana na taqwa na Iymaan zao.
- Mwenye kuwa na subra katika mitihani ndiye atakayepata kheri za Siku ya Qiyaamah na malipo mema kabisa, kinyume na atakayeshindwa kuwa na subra:
إِنَّمَا يُوَفَّى الصَّابِرُونَ أَجْرَهُم بِغَيْرِ حِسَابٍ
((Hakika wanaosubiri watalipwa kikamilifu ujira wao bila ya hesabu))[2]
- Muumin inampasa awe radhi kwa mitihani inayomfikia wala asikate tamaa au kuchukia bali ashukuru [Hadiyth: ((Ajabu ya jambo la Muumin kwamba kila jambo lake ni kheri. Na halipatikani hili isipokuwa kwa Muumin, Anapofikwa na jambo zuri hushukuru nayo ni kheri kwake, na anapofikwa na jambo lenye madhara husubiri, nayo ni kheri kwake))[3]
- Pepo si wepesi kuipata ila baada ya kuwa na taqwa, kutenda ‘amali njema na kuwa na subira katika mitihani. [Al-Baqarah 2: 214].
- Kuipita mitihani ni thibitisho kuwa mtu huyo yuwapendwa na Allaah (سبحانه وتعالى).
Subscribe to:
Comments (Atom)