2 Follow @BloggerSentral 3 4 FAHAD AHMAD: 2014

Tuesday, January 28, 2014

NIQAAB NDO VAZI LA PEKEE AMBALO HUMPA HESHMA YAKE KIUKAMILIFU



UISLAMU NA SUALA LA HIJABU-I

JIULIZE:
 1·NINI MTIZAMO WA UISLAMU KATIKA SUALA LA HIJABU KWA MWANAMKE NA HAKI YAKE YA KUSOMA NA KUFANYA KAZI.
 2·JE NI KWELI KUWA HIJABU HAIENDI SAMBAMBA NA MAISHA YA LEO? (IMEPITWA NA WAKATI).
Kwanza kabisa ni vema tukaelewa tunapozungumzia Hijabu tunazungumzia nini. Tunapoizungumzia Hijabu tunaikusuduia Hijabu kama ilivyo ndani ya Qur - ani Tukufu. Neno Hijabu limetumika ndani ya Qur - ani zaidi ya mara nane. Miongoni mwa aya zilizoitaja Hijabu ndani ya Qur - ani ni hizi zifuatazo:-
".. NANYI MNAPOWAULIZA (wakeze Mtume) WAULIZENI NYUMA YA PAZIA (Hijabu) ..." (33:53)
Hii ndio Hijaabu kwa lugha ya Qur - ani:-
"(NA WAKASEMA: "NYOYO ZETU ZI KATIKA VIFUNIKO KWA YALE UNAYOTUITIA; NA KATIKA MASIKIO YETU MUNA UZITO; NA BAINA YETU NA BAINA YAKO KUNA PAZIA. (Hijaabu) ???" (41:5)
Ione Hijaabu kupitia Qur - ani:-
"BASI AKASEMA ; NAVIPENDA VITU VIZURI KWA KUMKUMBUKA MOLA WANGU. KISHA (mafarasi) WAKAFICHIKANA NYUMA YA KIZIUIZI (Hijaabu, kwa kutiwa zizini mwao)" (38:32)
Ijue Hijaabu kupitia Qur-ani-
"NA AKAWEKA PAZIA (Hijaabu) KUJIJINGA NAO??.." 19:170.
Ielewe Hijaabu kupitia Qur-ani- "NA UNAPOSOMA QUR-ANI (inakuwa kama kwamba) TUMETIA BAINA YAKO NA BAINA YA WALE WASIOAMINI AKHERA PAZIA LILILOFUNIKWA (sana hata hawafahamu kinachosemwa)" (17:45)
Hizi ndizo baadhi ya aya za Qur-ani Tukufu ambazo ndani yake limetajwa na kutumika neno "Hijaabu". Kupitia aya hizi tunaweza kusema kuwa Hijaabu ya Kiislamu ni:-
a)Sitara ya kutokuchangayika pamoja wanume na wanawake.
b)Sitara ya kutokusikia sauti ya mwanamke kwa mwanamume.
c) Sitara ya mwili (mavazi) yaani kutoonekana mwili wa mwanamke ila na maharimu zake tu.
Hii ndio eleweko la Hijaabu kwa mtazamo wa kiislamu, kama tutakavyolithibitisha hilo na kulijengea hoja kupitia Qur-ani yenyewe. Hijaabu hailengi ila kuwa ni chombo cha kujenga na kuratibisha uhusiano mwema uliopo baina ya jinsia mbili zihitajianazo na kutegemeana, mwanamume na mwanamke. Huu ni utaratibu na nidhamu ya lazima inayozisaidia jinsia mbili hizi kuistawisha dunia na kuyafurahia maisha katika misingi waliyowekewa na Mola Muumba wao. Kila mmoja, mwanamume na mwanamke ameamrishwa na kukalifishwa kuishi kwa kuufuata utaratibu na nidhamu hii. Hii ni kwa ajili ya kuidhibiti na kuitawala nguvu ya kimaumbile iliyopo baina ya jinsia mbili hizi. Nguvu ambayo ina athari kubwa katika kuvuruga na kuharibu mwenendo na silka nzima ya mwanadamu. Mvuto na matamanio ya kijinsia alio nayo mwanamume, yanapatikana pia kwa mwanamke. Kila mmoja kwa mwenzie ni mfano wa sumaku inayokivuta chuma na hatimaye kukinasa na kushikamana nacho. Haya ndio maumbile yaliyokamilika na chanzo/sababu yake ya msingi ni "Homonsi" alizoumbiwa kila mmoja wao. Ni kwa kulijua na kuzingatia tabia hii ya maumbile ya mwanadamu ndio tunaikuta Hijaabu hata katika vilabu vya Mwenyezi Mungu Mtukufu vilivyoitangulia Qur-ani.
Hijaabu ya Kiislamu haikomelei tu katika kusitiri na kuhifadhi mapambo (sehemu zenye kuamsha na kuchochea fitna kati ya mwanamume na mwanamke), na kuinamisha macho tu bali Hijaabu ni pamoja na:-
 1·Kutokukaa faraghani mwanamume na mwanamke. Haya ndiyo maelekezo na mafundisho ya Bwana Mtume- Rehema na Amani zimshukie - kupitia kauli yake:-"Asikae, asikae, rafaghani mmoja wenu na mwanamke ila (awe pamoja na mwanamke huyo) maharimu (yake, baba, kaka, babu n.k). Bukhariy na Muslim.
 2·Kutogusana mwili na mwanamume na mwanamke. Haya ndio mafundisho ya Uislamu kupitia kauli ya Mtume wa Uislamu- Rehema na Amani zimshukie:- "Mmoja wenu kuchomwa kichwani kwake na sindano ya chuma na bora kwake kuliko kumgusa mwanamke asiye halali yake" Twabaraany. Amesema mkewe Bwana Mtume , Bi Aysha- Allah amuwiye radhi: "Wallah! Mkono wa Mtume wa Mwenyezi Mungu Haukupata kabisa kumgusa mwanamke (asiye halali yake), ila alikuwa akipeana nao ahadi kwa maneno (kwa kuzungumza) tu"
 3·Mwanamke kutokulegeza sauti yake mbele ya mwanamume. Tusome: ENYI WAKE WA MTUME, NINYI SI KAMA YOYOTE TU KATIKA WANAWAKE WENGINE (ninyi wakeze Mtume). KAMA MNATAKA (kufanya jambo la) KUMCHA ALLAH, BASI MSILEGEZE SAUTI (zenu mnaposema na wanaume) ILI ASITAMANI MTU MWENYE UGONJWA MOYONI MWAKE (kufanya mabaya na nyie) NA SEMENI MANENO MAZURI " (33:32). Semezo (kihitwaabu) la aya hii linaelekezwa moja kwa moja kwa wakeze Bwana Mtume lakini amri hii inawahusu na kuwaenea wanawake wote wa Kiislamu.
 4·Kuzuia picha, magazeti, majarida, vipeperushi, nakala na matangazo ambayo kwa namna moja au nyingine huchochea na kuamsha tmaa na matamanio ya kimwili.
 5·Mwanamke kujitia manukato na kupita mbele ya wanaume . Bwana Mtume - Rehema na Amani zimshukie - anatahadharisha juu ya hili kwa kutuambia "Mwanamke yeyote atakayejitia manukato na kupita mbele ya wanamume ili waipate harufu ya (manukato) yake, basi mwanamke huyo ni mzinifu (anapata dhambi za kuzini kwa sababu ya kushawishi kwake zinaa) na kila jicho (limtazamalo) pia ni zinifu" Abuu Daawoud, Tirmidhiy, Nasaai, Ibn Khuzaymah na Ibn Hibban.
Haya ni baadhi tu ya maeneo yanayoguswa moja kwa moja na Hijaabu ya Kiislamu. Msingi na asili ya suala la Hijaabu ni kauli tukufu ya Mwenyezi Mungu Mtukufu ndani ya Qur-ani Tukufu isemayo "NA WAAMBIE WAISLAMU WANAWAKE WAINAMISHE MACHO YAO, NA WAZILINDE TUPU ZAO WALA WASIDHIHIRISHE VIUNGO VYAO ISIPOKUWA VINAVYODHIHIRIKA (nao ni uso na vitanga vya mikono). NA WAANGUSHE SHUNGI ZAO MPAKA VIFUANI MWAO, NA WASIONYESHE MAPAMBO YAO ILA KWA WAUME ZAO, AU BABA ZAO, AU BABA ZA WAUME ZAO (wakwe zao) AU WATOTO WAO, AU WATOTO WA WAUME ZAO, AU KAKA ZAO, AU WANA WA KAKA ZAO, AU WANA WA DADA ZAO, AU WANAWAKE WENZIWAO, AU WALE ILIYOWAMILIKI MIKONO YAO YA KIUME (watumwa wao) AU WAFUASI WANAUME WASIO NA MATAMANIO ( kwa wanawake) AU WATOTO AMBAO HAWAJAJUA MAMBO YANAYOHUSU UKE, WALA WASIPIGE MIGUU YAO ILA YAJULIKANE WANAYOYAFISHIA KATIKA MAPAMBO YAO NA TUBIENI NYOTE KWA ALLAH ENYI WAISLAMU ILI MPATA KUFAULU" (24:31).
Alisema Bwana Mtume - Rehema na Amani zimshukie - wakati Asmaa Bint Abuu Bakri - Allah awawiye radhi wote - alipoingia kwa Mtume akiwa amevaa nguo nyepesi: "Ewe Asmaa, hakika mwanamke anapofikilia umri wa kupata hedhi (anapovunja ungo) haifai kuonekanwa (mwili) wake ila hiki na hiki. Na (Mtume) akaashiria uso na vitanga vyake" Abuu Daawoud.
Miongoni mwa sharti za Hijaabu ya vazi la mwanamke wa Kiislamu ni kwamba:-
a)Isiwe nguo yenyewe ni pambo linaloweza kumvutia mtazamaji. Hilo ndilo eleweko na fahamisho la kauli ya Allah isemayo" "WALA WASIDHIHIRISHE MAPAMBO YAO??." (24:31) Na kauli isemayo, "NA KAENI MAJUMBANI MWENU, WALA MSIONYESHE MAPAMBO YENU KAMA WALIVYOKUWA WAKIONYESHA MAPAMBO YAO WANAWAKE WA ZAMA ZA UJAHILI (Ujinga ukafri)??.' (33:33).
b)Iwe nzito isiwe nyepesi ionyeshayo rangi ya mwili. Hii ni kutokana na kauli ya Mtume isemayo:" Watakuwepo mwisho wa umati wangu wanawake watakaovaa (lakini) wako uchi. Vichwani mwao kuna nundu (kutokana na mitindo ya nywele) kama nundu za ngamia. Walaanini kwa kuwa wao wamelaaniwa??" Ahmad.
c)Isiwe yenye kubana sana kiasi cha kuonyesha ramani/finyango la mwili.
d)Isiwe imetiwa manukato au kufukizwa kwa udi, Haya ni kwa mujibu wa kauli ya Bwana Mtume - Rehema na Amani zimshukie aliposema" Mwanamke yeyote atakayejitia manukato, kisha akapita mbele ya wanaume ili waipate harufu yake, basi yeye ni mzinifu",
e)Isifanane na nguo za wanaume, hivyo ndivyo tunavyofahamu kutokana na kauli ya Bwana Mtume - Rehama na Amani zimshukie - isemayo: "Si katika sisi mwanamke mwenye kujishabihisha na wanaume wala mwanaume mwenye kujishabihisha na wanawake. Twabaraaniy na Ahmad.

HAKI YA JIRANI

Tuanze na kujiuliza, jirani ni nani? Jirani tunayemkusudia hapa ni yule mtu aliye karibu yako kimakazi, yaani nyumba zenu zinakurubiana. Mtu mwenye wasifu huu ana haki kubwa juu yako, ewe muislamu. Itakaposadifu kwamba jirani yako ni ndugu yako wa nasabu na akawa ni muislamu mwenzako. Basi jirani huyu atakuwa ana haki tatu kwako; haki ya ujirani, haki ya udugu na haki ya Uislamu. Na akiwa jirani yako ni muislamu lakini si nduguyo wa nasabu, huyu atakuwa nazo kwako haki mbili; haki ya ujirani na haki ya Uislamu. Na iwapo jirani yako huyu si muislamu na hapana udugu baina yenu, jirani huyu atamiliki kwako haki moja tu nayo ni haki ya ujirani. Hivi ndivyo anavyotufundisha Mtume wa Allah-Rehema na Amani zimshukie: “Majirani ni watatu; jirani mwenye haki moja naye ndiye mwenye haki ndogo kuliko wote. Na jirani mwenye haki mbili na jirani mwenye haki tatu. Ama yule ambaye mwenye haki moja ni jirani mushriki (kafiri), na ama ambaye mwenye haki mbili ni jirani muislamu (ana) haki ya Uislamu na haki ya ujirani. Na ama yule mwenye haki tatu ni jirani muislamu aliye ndugu, (ana) haki ya Uislamu, haki ya ujirani na haki udugu”. Al-Bazzaar & Abuu Nuaim.
Muislamu anakiri, anaikubali na kuichunga haki ya jirani akiamini kuwa kufanya hivyo ni kuitekeleza amri ya Mola wake: “MWABUDUNI ALLAH WALA MSIMSHIRIKISHE NA CHO CHOTE NA WAFANYIENI IHSANI WAZAZI WAWILI NA JAMAA NA MAYATIMA NA MASKINI NA JIRANI WALIO KARIBU NA JIRANI WALIO MBALI--- [ 4 : 36] Naye Mtume wa Allah–Rehema na Amani zimshukie-kama mfasiri mkuu wa Qur–ani, anauelezea uzito wa haki hii ya jirani iliyotajwa ndani ya Qur-ani anasema: “Hakuacha Jibril kuniusia juu ya jirani mpaka nikadhani kwamba atampa na haki ya kurithi”. Bukhaariy & Muslim.
Miongoni mwa haki za jirani kama zilivyoelezwa na Uislamu ni kumtendea wema kiasi cha uwezo wa mtu. Mtendee wema jirani yako kwa mali yako, cheo chako na kila chako chenye kuweza kumnufaisha kwa namna moja au nyingine. Hivi ndivyo anavyo tufundisha. Mtume wa Allah–Rehema na Amani zimshukie– kutokana na kauli yake: “Jirani bora mbele ya Allah ni yule aliye mwema kwa jirani yake”. Tirmidhiy.
Na akasema tena Bwana Mtume: “Mwenye kumuamini Allah na siku ya mwisho basi na amtendee wema jirani yake”. Muslim.
Kauli hii ya Mtume wa Allah kama inafahamisha jambo, basi jambo hilo si jingine bali ni kuwa ukitaka kumjua muumini wa kweli basi muangalie anavyoishi na jirani yake. Imepokelewa kutoka kwa Muawiyah Ibn Jundub-Allah amuwiye radhi–kwamba alimuuliza Mtume wa Allah–Rehema na Amani zimshukie: “Ewe Mtume wa Allah, ni ipi haki ya jirani kwa jirani yake? Mtume akamjibu:-
Akiugua mkague (mtake hali),
Akifa msindikize (nenda kamzike),
Akikuomba mkopo, mkopeshe,
Akienda utupu (hana nguo), msitiri ( mvike ),
Akipatwa na kheri, mpongeze,
Akipatwa na msiba, muizi (mfanyie ta’azia),
Wala usinyanyue nyumba yako zaidi kuliko nyumba yake ukamzibia hewa/upepo,
Na wala usimuudhi kwa harufu ya chungu chako ila umchotee kidogo”. Twabaraaniy
Kumtendea wema jirani alikokueleza Bwana Mtume katika hadithi tulizozitaja ni pamoja na kumpelekea zawadi katika furaha mbali mbali anazozipata. Mithili ya kufaulu katika mtihani, kupata cheo, kuzaliwa mtoto, kuoa/kuozesha, kujenga nyumba na kadhalika. Falsafa na siri ya kupeana zawadi ni kujenga mapenzi na kuondosha chuki na uadui kama anavyolibainisha hilo Mtume wa Allah–Rehema na Amani zimshukie: “Peaneni zawadi mtapendana, na peaneni mikono itakuondokeeni chuki baina yenu”. Ibn Asaakir.
Na katika jumla ya haki za jirani ni kutokumuudhi kwa kauli au matendo. Siku moja Mtume wa Allah–Rehema na Amani zimshukie– alisema: “Wallahi hawi muumini, Wallahi hawi muumini, Wallahi hawi muumini. Maswahaba wakamuuliza: Ni nani huyo ewe Mtume wa Allah? Akajibu: Huyo ni yule ambaye jirani yakke hasalimiki na shari/uovu wake”. Bukhaariy
Mtu mmoja alimuendea Mtume wa Allah na kumuambia: “Hakika mwanamke fulani anatajwa sana kwa wingi wa swala zake, kutoa kwake sadaka kwa wingi na wingi wa kufunga kwake. Isipokuwa kwamba yeye anamuudhi jirani yake kwa ulimi wake. Mtume akasema: “(Pamoja na ibada zake zote hizo, mwanamke) huyo ataingia motoni”. Ahmad, Al-Bazzaar, Ibn Hibbaan & Al-haakim.
Kauli hii ya Mtume wa Allah inaonyesha uzito wa dhambi ya kumuudhi jirani na kwamba ibada ya mtu anayemfanyia maudhi jirani yake haitamsaidia kuingia peponi jirani huyo mbaya. Na kinyume chake, kutokumuudhi jirani ni sababu tosha inayoweza kumuingiza mtu peponi, kwani kukaa kwa wema na jirani bila ya kumuudhi kwa maneno au matendo ni kielelezo cha wema wa mja. Imepokelewa kwamba mtu mmoja alimwambia Mtume wa Allah– Rehema na Amani zimshukie–nijulishe amali ambayo nitakapoitenda nitaingia peponi. Mtume akamjibu: “Kuwa mwema”. Akasema mtu yule: Ewe Mtume wa Allah, nitajuaje kwamba mimi ni mwema?
Mtume akamwambia: Waulize jirani zako, wakikuambia kwamba wewe ni mtu mwema basi fahamu kwamba wewe ni mwema (kweli). Na wakikuambia kwamba wewe ni mtu mbaya (muovu), basi fahamu kwamba wewe ni mbaya (kweli )”. Al-Baihaqiy
Huyu ndiye jirani na haki yake katika Uislamu, lakini watu wengi miongoni mwetu hawaijali haki hii ya ujirani. Kutokuitambua haki hii ya ujirani ndio imekuwa sababu kuu ya magomvi uadui na mizozo mitaani mwetu. Utawaona majirani daima wakigombana kwa mambo ya kipuuzi kabisa kiasi cha kuwafanya wasijuliane hali na kutokushirikiana katika furaha wala huzuni. Huu si Uislamu aliokuja nao Bwana Mtume kutoka kwa Allah, muislamu wa kweli haishi hivyo na jirani yake hata kama si muislamu mwenziwe(kafiri )

KUJIZUIA NA HARAMU NA MAMBO MACHAFU

Chimbuko na chemchem ya somo letu hili linalobeba anuani ya kujizuia na haramu/mambo machafu ni kauli yake MwenyeziMungu aliposema :
“NA WAJIZUILIYE NA MACHAFU WALE WASIOPATA CHA KUOLEA MPAKA AWATAJIRISHE KATIKA FADHILA ZAKE …..” [24:33]
Kujizuia na haramu/mambo machafu ni nguvu na uwezo uliomo ndani ya nafsi ya binadamu wa kuyadhibiti na kuyashinda matashi na matamanio ya nafsi yake yasimpondoe na njia ya MwenyeziMungu, ambayo ghalibu/mara nyingi ndio kazi ya nafsi kama tunavyosoma :
“NAMI SIJITAKASI NAFSI YANGU; KWA HAKIKA (kila) NAFSI NI YENYE KUAMRISHA SANA MAOVU, ISIPOKUWA ILE AMBAYO MOLA AMEIREHEMU….” [12:53]
Kuizuia nafsi na mambo yaliyoharamishwa ambayo mengine hujidhihirisha katika sura ya mvuto na ladha kiasi cha kuichukua mateka nafsi ya mwanadamu, ni miongoni mwa mambo na sifa tukufu anazotakiwa kupambika nazo mwanadamu ili apate kuushinda ule unyama alioumbiwa na kuwa mtu mkamilifu wa utu na ubinadamu. Mwanadamu akiweza kufika hapo kwa kuyashinda matashi na matamanio ya nafsi yake basi atakuwa amejihakikishia kufaulu leo ulimwenguni na kesho akhera. Haya yamethibitishwa na maneno matukufu ya MwenyeziMungu :
“NA KWA NAFSI NA ALIYEITENGENEZA. KISHA AKAIFAHAMISHA UOVU WAKE NA WEMA WAKE. BILA SHAKA AMEFAULU ALIYEITAKASA (nafsi yake). NA BILA SHAKA AMEJIHASIRI ALIYEUZA (nafsi yake) [91:7-10]
Kutokana na aya hizi tunatambua kuwa kumbe nafsi ya mwanadamu tayari imekwishapewa uwezo na ujuzi wa kujua jema na baya na kisha ikaachiwa uhuru wa kuchagua kufuata jema au baya/ovu ili ikalipwe kesho akhera kwa mujibu wa uchaguzi ilioufanya hapa duniani. Qur-ani inatuambia :
“HAKIKA SISI TUMEMUONGOZA (tumembainishia) NJIA (zote mbili: kuwa hii ndiyo ya kheri na hii ndiyo ya shari) BASI (mwenyewe tena) ATAKUWA MWENYE SHUKRANI AU AWE MWENYE KUKUFURU (kukanusha)” [76:3]
Uwezo wa kujizuia na haramu/ mambo machafu huzaa tabia njema na nzuri, uwezo huu humfanya mwanadamu awe na subira kwa maana ya subira ya kweli. Aweze kusubiri kuyashinda maovu na kuendelea kusubiri katika kutenda mema ambayo mara nyingi nafsi huyaona kuwa ni magumu na mazito. Humpa mwanadamu kukinai na kutosheka na kile alichokadiriwa na kupewa na Mola wake, jambo ambalo ni utajiri mkubwa kama alivyosema Bwana Mtume –Rehma na amani zimshukie –
“Utajiri si (mtu) kuwa na mali nyingi lakini utajiri ni utajiri wa nafsi (ya mtu kutosheka)” Ahmad, Muslim, na Tirmidhi.
Kujizuiya na haramu humfinyanga mwanadamu kuwa mkarimu na mpaji. Kwa ujumla tunaweza kusema nguvu na uwezo huu wa kuidhibiti nafsi isifuate matashi na matamanio yake ni KHAZINA ya asokuwa na mali na ni taji la asokuwa na utukufu.
Hebu na tujiulize basi ni nini sababu ya utukufu huu au mwanadamu afanye nini hata aweze kuifikia daraja hii tukufu ambapo ataweza kuwa juu ya nafsi yake akaweza kuitawala na sio nafsi kumkalia mbele na kumburuzia ? Mwanadamu hawezi kukifikia kilele hiki ila kwa kuachana na :
 Tamaa mbaya. Bwana Mtume –Rehma na amani zimshukie – anatuasa : “Jilindeni kwa Allah kutokana na tamaa yenye kupelekea katika chuki/ghadhabu na (kutokana) na tamaa iongozayo kwenye kisichotumainiwa na (kutokana) na kutamani pasipo na matumaini”. Ahmad,Al-twabraaniy na Al-haakim.
 Pupa katika kuchuma mali : Hili ndio mama wa maovu yote, kwa sababu mwanadamu anapokuwa lengo lake ni kujikusanyia na hatimaye kujilimbikizia mali kwa kuichelea umasikini, basi sera zake huwa ni kupata tu bila kuzingatia anapata kwa njia gani, ya halali au ya haramu. Katika hali hii mwanadamu huyu yuko tayari kukabiliana na kikwazo chochote kinachoweza kumzuia asifikie lengo lake; hata ikibidi kuitoa roho ya mwanadamu mwenziwe ndipo apate, basi yuko tayari kufanya hivyo kwa gharama yeyote ile. Mtume wa MwenyeziMungu – Rehma na amani zimshukie – anatuhadharisha : “Hakika kila umati una fitna yake na fitna ya umati wangu ni mali” Al-tirmidhi, Ibn Hibbaan, na Al-Haakim.
 Kuridhia na kichache unachokipata. Amesema Bwana Mtume – Rehma na amani zimshukie – “Bila ya shaka amefaulu aliyejinyenyekesha kwa Mola wake na akaruzukiwa chenye kumtosha na MwenyeziMungu akamkinaisha na alichompa” Ahmad, Muslim, Al-tirmidhi, na Ibn Maajah.
Mwanadamu hawezi kuifikia daraja ya kujizuia na haramu/mambo machafu kwa ukamilifu, mpaka pale atakapoweza kuukemea na kuuzuia ulimi wake, macho, masikio, tumbo na baki ya viiungo vyake vingine vya mwili. Asiunyooshe mkono wake katika kutoa au kupokea rushwa, asiutumie mkono wake kumdhuru mtu bila ya haki, asiutumie ulimi wake kutukana, kufitinisha, kusengenya, kusema uongo, kutoa ushahidi wa uongo na kama hayo. Ayazuiliye masikio yake kusikiliza maneno machafu ya kipuuzi na kila kilichoharimishwa kukisikiliza. Macho yake yasiwaangalie wanawake/wanaume wasio halali yake, asivikodolee macho ya tamaa vilivyomo mikononi mwa watu, asiwatizame watu kwa jicho la dharau. Asiliruhusu tumbo lake kula riba, mali ya yatima na chochote kile kilichoharimishwa. Asiitumie tupu (uchi) yake mahala pasipo halali yake. Ili mradi anatakiwa akizuie kila kiungo chake na kila lililoharamishwa na kukatazwa huku akiitafakari kauli ya Mola wake :
“HAKIKA MASIKIO NA MACHO NA MOYO; HIVYO VYOTE VITAULIZWA” [17:36]
Mtume wa MwenyeziMungu – Rehma na amani zimshukie – anatuambia “Ukiwa nayo mambo matatu basi hakikudhuru kilichokufutu/kilichokupita katika dunia; ukweli wa mazungumzo, kuhifadhi amana na kujizuia na tamaa”

TUJIFUNZE NA TUKUBALI KUWA : Dini ni tabia njema, ndio maana Bwana Mtume anatuambia sababu ya kuletwa kwake kwa kusema : “Hakika si vinginevyo, sikutumilizwa ila kuja kukamilisha tabia njema” Ibn Sa’d, Al-Bukhariy, Al-Haakim, na Al-Bayhaqiy.
Sote tunakubali kuwa KUKAMILISHA sio kuasisi wala kuanzisha, kwa msingi huu tunaelewa kuwa Bwana Mtume hakuja kuasisi kitu kipya bali amekuja kumalizia kazi iliyoasisiwa na nduguze mitume waliotangulia kabla yake.
Miongoni mwa tabia njema unazopaswa kupambika nazo ni hii ya kujizuia na haramu/mambo machafu. Anza sasa kusema na kuikemea nafsi yako na shetani, huku ukitambua kuwa wawili hao ndio maadui zako wakubwa.
“KWA YAKINI SHETANI NI ADUI YENU, BASI MFANYENI ADUI (yenu: kwa hiyo msimtii) KWANI ANALIITA KUNDI LAKE LIWE KATIKA WATU WA MOTONI” [35:6]

KUTEKELEZA AHADI

i/ Kutekeleza ahadi ni miongoni mwa tabia njema/tukufu anazotakiwa ajipambe nazo muislamu wa kweli. Muislamu anapotoa ahadi, basi atambue kwamba amelazimishwa na sheria kuitekeleza ahadi muda wa kuwa si katika kumuasi Mola Mtukufu. Mwenyezi Mungu atuambia:-"NA TIMIZENI AHADI. KWA HAKIKA AHADI ITAULIZWA (siku ya kiama) (17:34)
Kukhalifu au kutokutimiza ahadi ni katika jumla ya alama za unafiki wa mtu kama anavyotubainishia hilo Bwana mtume: "Alama za mnafiki ni tatu:anapozungumza husema uwongo, na akiahidi hukhalifu (hatekelezi ahadi) na akiaminiwa hufanya khiyana". Bukhaariy na muslimu.
Tabia ya kutekeleza ahadi humfanya mtu aaminiwe na watu, atajwe vema katika uhai na baada ya kufa kwake kama Qur-ani inavyotuambia:
"NA MTAJE KATIKA KITABU (hiki) ISMAIL. BILA SHAKA YEYE ALIKUWA MKWELI WA AHADI, NA ALIKUWA MTUME, NABII". (19:54)
Mwenyezi Mungu amuambia Nabii Muhammad amtaje na kumkumbuka Mtume wake Ismail ndani ya Qur-ani baada ya kupita chungu ya miaka kwa sababu ya kupambika kwake na tabia tukufu ya kutekeleza ahadi. Anayetoa ahadi na kutimiza basi atambue kwamba amepambika na sifa miongoni mwa sifa za mitume. Sifa hii kutekeleza ahadi huambatana na sifa mbili kuu; kusema ukweli na kutokukhini amana. Basi ukimuona mtu atekeleza ahadi basi mshuhudie pia kuwa ni mkweli asiye na khiyana.
ii/ UKWELI
Ukweli ni mtu kulieleza jambo kama kilivyo bila yakupunguza au kuzidisha chochote.
Muislamu huwa ni mkweli apendaye kusema ukweli na kujitazamisha na tabia ya ukweli hii ni kwa sababu anatambua ukweli humuongezea katika wema, wema ambao humuongoza (kumpeleka) peponi na pepo ndio lengo kuu la muislamu. Muislamu hauangalii ukweli kama ni tabia njema anayopaswa kujipamba nayo tu bali huenda mbali zaidi ya hapo. Huuona ukweli kuwa ni miongoni mwa mambo yanayoikamilisha imani na uislamu wake: Mwenyezi Mungu anatuagiza:-
"ENYI MLIOAMINI: MCHENI ALLAH NA KUWENI PAMOJA NA WAKWELI" (9:119)
Ukweli umejengeka juu ya sababu tatu, ambazo ni:-
 Akili – akili timamu ndio humfanya mtu anayetambua manufaa ya ukweli na madhara ya uwongo.
 Murua – mtu mwenye murua, murua wake haumruhusu na kumuachia kusema uwongo bali humlazimisha ajipambe na tabia ya ukweli
 Dini – Dini pia humfinyanga mtu ksema ukweli kwa kuamini kuwa dini inamuamrisha kusema ukweli na inamkataza kusema uwongo.
Ukweli pia ni miongoni mwa sifa njema walizopambika nazo Mitume wa Mwenyezi Mungu. Qur-ani yatuambia:- "NA MTAJE IDRIS KATIKA KITABU (hiki). BILA SHAKA YEYE ALIKUWA MKWELI SANA NA NABII". (19:56)
Tabia ya ukweli huzaa matunda mema na mazuri ambayo huvunwa na watu wakweli. Miongoni mwa matunda hayo ni:-
 Utulivu wa nafsi – Mwenye kupambika na tabia ya ukweli huwa na utulivu wa nafsi kwa mujibu wa kauli ya Mtume: "Ukweli ni utulivu" – At-tirmidhiy
 Baraka katika chumo na ziada ya kheri – Bwana Mtume amesema: "Wauzianaji(Muuzaji na mnunuzi) wana khiyari (ya kupitisha au kuvunja biashara) muda wa kuwa hawajatengana, wakiwa wakweli na wakabainisha (aibu za kinachouzwa) watabarikiwa katika biashara yao, na wakificha (aibu) na wakasema uongo itafutwa baraka ya biashara yao" Al-bukhaariy
 Kufuzu kwa kupata daraja ya mashahidi, hili linathibitishwa na kauli ya Mtume aliposema: "Mtu atakayemuomba Mwenyezi Mungu kufa shahidi kwa ukweli, Mwenyezi Mungu atamfikisha daraja ya mashahidi hata akifia kitandani". Muslim
 Kuepuka balaa, inasimuliwa kwamba mtu mmoja aliyekuwa anakimbizwa alikimbilia kwa mtu mwema mmoja akamuomba amfiche hasikamatwe. Yule mtu mwema akamwambia; "Lala hapa", akamfunika na rundo la makuti. Wale waliokuwa wanamkimbiza wakapita pale kwa yule mtu mwema wakamuuliza :"Umemuona mtu akipita hapa anakimbia?" Akawajibu: "Huyo hapo chini ya makuti". Wale watu wakamuona nawafanyia maskhara wakampuuza wakaenda zao. Yule mtu aliyekuwa akikimbizwa akaokoka kwa bababu ya ukweli wa mtu mwema yule.
 Kuchuma mapenzi ya Mola na watu. Mtu mkweli hupendeza mbele ya Mwenyezi Mungu na watu na watu wema humpenda.

Friday, January 17, 2014

Allaah Akimtakia Kheri Mja Humpa Mtihani Duniani


عَنْ أَنَسٍ (رضي الله عنه) قَال: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ (صلى الله عليه و آله وسلم): ((إِذَا أَرَادَ اللَّهُ بِعَبْدِهِ الْخَيْرَا عَجَّلَ لَهُ الْعُقُوبَةَ فِي الدُّنْيَا وَإِذَا أَرَادَ اللَّهُ بِعَبْدِهِ الشَّرَّ أَمْسَكَ عَنْهُ بِذَنْبِهِ حَتَّى يُوَافِيَ بِهِ يَوْمَ الْقِيَامَةِ)) وَ قال النَّبِيِّ (صلى الله عليه و آله وسلم): ((إِنَّ عِظَمَ الْجَزَاءِ مَعَ عِظَمِ الْبلآءِ وَإِنَّ اللَّهَ إِذَا أَحَبَّ قَوْمًا ابْتَلاَهُمْ فَمَنْ رَضِيَ فَلَهُ الرِّضَا وَمَنْ سَخِطَ فَلَهُ السَّخَطُ)) رواه الترمذي وقال حديث حسن
Imepokelewa kutoka kwa Anas (رضي الله عنه)  amesema: Mtume wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Allaah Anapompendelea mja Wake kheri, Humharakishia adhabu duniani. Na Allaah Anapomtakia mja Wake shari, Humzuilia dhambi zake mpaka Amlipe Siku ya Qiyaamah)). Na amesema Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم): ((Hakika malipo makubwa kabisa yapo pamoja na mtihani mkubwa, na hakika Allaah Anapowapenda watu Huwapa mtihani. Basi atakayeridhika, atapata Radhi [za Allaah] na atakayechukia, atapata hasira. [za Allaah]))[1]
 
Mafunzo Na Hidaaya: 
 
  1. Allaah (سبحانه وتعالى) Huwa pamoja na anayesibiwa na mitihani akasubiri, na juu ya hivyo, ni alama ya mapenzi ya Allaah (سبحانه وتعالى). [Aal-‘Imraan 3: 146, Al-Baqarah 2: 153, Al-Anfaal 8: 46].
 
  1. Alama za kufutiwa dhambi Muislamu anapokuwa na subra katika mitihani.
 
  1. Watu hupewa mitihani kulingana na taqwa na Iymaan zao.
 
  1. Mwenye kuwa na subra katika mitihani ndiye atakayepata kheri za Siku ya Qiyaamah na malipo mema kabisa, kinyume na atakayeshindwa kuwa na subra: 
 
 
إِنَّمَا يُوَفَّى الصَّابِرُونَ أَجْرَهُم بِغَيْرِ حِسَابٍ
((Hakika wanaosubiri watalipwa kikamilifu ujira wao bila ya hesabu))[2]
 
  1.  Muumin inampasa awe radhi kwa mitihani inayomfikia wala asikate tamaa au kuchukia bali ashukuru [Hadiyth: ((Ajabu ya jambo la Muumin kwamba kila jambo lake ni kheri.  Na halipatikani hili isipokuwa kwa Muumin, Anapofikwa na jambo zuri hushukuru nayo ni kheri kwake, na anapofikwa na jambo lenye madhara husubiri, nayo ni kheri kwake))[3]
 
  1. Pepo si wepesi kuipata ila baada ya kuwa na taqwa, kutenda ‘amali njema na kuwa na subira katika mitihani. [Al-Baqarah 2: 214].
 
  1. Kuipita mitihani ni thibitisho kuwa mtu huyo yuwapendwa na Allaah (سبحانه وتعالى).
 

Allaah Hupokea Tawbah Za Waja Usiku Na Mchana



عَنْ أَبِي مُوسَى عَبْدِ الله بنِ قَبَسٍ الأَشْعَرِيِّ  (رضي الله عنه) عن النَّبيّ (صلى الله عليه و آله وسلم) قال: ((إِنَّ اللَّهَ تَعَالَى يَبْسُطُ يَدَهُ بِاللَّيْلِ لِيَتُوبَ مُسِيءُ النَّهَارِ وَيَبْسُطُ يَدَهُ بِالنَّهَارِ لِيَتُوبَ مُسِيءُ اللَّيْلِ حَتَّى تَطْلُعَ الشَّمْسُ مِنْ مَغْرِبِهَا)) رواه مسلم
Imepokelewa kutoka kwa Abu Muwsaa ‘Abdillaah bin Qays Al-Ash‘ariyy (رضي الله عنه)  kwamba Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Hakika Allaah Anakunjua Mkono Wake usiku ili Apokee tawbah ya mkoseaji mchana. Na Anakunjua Mkono Wake mchana ili Apokee tawbah ya mkoseaji usiku mpaka jua lichomoze Magharibi [mahali linapokuchwa]))[1]
 
Mafunzo Na Hidaaya:
 
  1. Umuhimu wa mja kukimbilia kutubu anapofanya maasi mchana au usiku. [At-Tahriym 66: 8, An-Nuwr 24: 31].
 
وَسَارِعُوا إِلَىٰ مَغْفِرَةٍ مِّن رَّبِّكُمْ وَجَنَّةٍ عَرْضُهَا السَّمَاوَاتُ وَالْأَرْضُ أُعِدَّتْ لِلْمُتَّقِينَ
Na kimbilieni maghfirah kutoka kwa Mola wenu na Jannah upana wake ni wa mbingu na ardhi imeandaliwa kwa wenye taqwa[2]
 
  1. Rahma ya Allaah (سبحانه وتعالى) kwa waja Wake kuwapa muda wa kutubia maasi, lau sivyo Angeliwaadhibu na kuwaangamiza hapo hapo wanapotenda maasi. [Faatwir 35: 45, An-Nahl 16: 61].
 
  1. Rahma ya Allaah kwa waja Wake kutokutofautisha wakati wa tawbah japokuwa maasi mengine yanazidi mengineyo. 
 
  1.  Tawbah inaendelea kupokelewa hadi milango ifungwe: [Hadiyth: ((Hakika Allaah Huikubali tawbah ya mja Wake kabla ya roho kufika kwenye mkoromo wa mauti))[3] ((Atakayetubu kabla ya kuchomoza jua upande wa Magharibi, Allaah Atamkubalia tawbah yake)).[4]
 
  1. Hii inaonyesha mahaba makubwa ya Allaah (سبحانه وتعالى) kwa kuwapatia fursa hii ya dhahabu ambayo haifai kupotezwa na waja wenyewe.
 
  1. Hadiyth inatoa mafunzo kwa Muislamu kutokumhukumu mwenziwe kuwa hatoghufuriwa madhambi yake. [Rejea Hadiyth namba 99].
 
  1. Mja hata afanye madhambi makubwa vipi, asikate tamaa na Rahma ya Allaah (سبحانه وتعالى), kwani Yeye Hughufuria madhambi yote. [Az-Zumar 39: 53]

Allaah Hatazami Miili Wala Sura, Bali Anatazama Nyoyoni



عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ (رضي الله عنه)  قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ  (صلى الله عليه و آله وسلم): ((إِنَّ اللَّهَ لاَ يَنْظُرُ إِلى أجْسَامِكُمْ  وَلاَ إِلَى صُوَرِكُمْ وَلَكِنْ يَنْظُرُ إِلَى قُلُوبِكُمْ)) رواه مسلم
Imepokelewa kutoka kwa Abu Hurayrah (رضي الله عنه) amesema: Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Hakika Allaah Hatazami viwiliwili vyenu wala sura zenu, lakini Anatazama nyoyo zenu))[1]
 
Mafunzo Na Hidaaya:
 
  1. Umuhimu wa kuwa na niyyah safi na ikhlaasw katika kumuabudu Allaah (سبحانه وتعالى) kwani hivyo ndivyo tulivyoamrishwa:
 
وَمَا أُمِرُوا إِلَّا لِيَعْبُدُوا اللَّـهَ مُخْلِصِينَ لَهُ الدِّينَ حُنَفَاءَ وَيُقِيمُوا الصَّلَاةَ وَيُؤْتُوا الزَّكَاةَ ۚ وَذَٰلِكَ دِينُ الْقَيِّمَةِ
 Na hawakuamrishwa ila kumwabudu Allaah kwa kumtakasia Dini, hunafaa [wakielemea Dini ya haki na kuacha Dini potofu] na wasimamishe Swalaah, na watoe Zakaah, na hiyo ndiyo Dini iliyo sawa[2]
 
  1. Hima ya kutenda ‘amali njema baada ya kuwa na  niyyah safi.
 
  1. ‘Amali na ‘Ibaadah hazipokelewi isipokuwa niyyah ikiwa ni safi kwa ajili ya Allaah (سبحانه وتعالى) [Al-Kahf 18: 103-104, 110, Al-Furqaan 25: 23].
 
  1. Hakuna ajuaye yaliyo moyoni mwa mja isipokuwa Allaah (سبحانه وتعالى) [Al-Mulk 67: 13, Huwd 11: 5, Faatwir 35: 38, Al-Hadiyd 57: 6, At-Taghaabun 64: 4].
 
يَعْلَمُ خَائِنَةَ الْأَعْيُنِ وَمَا تُخْفِي الصُّدُورُ
(([Allaah] Anajua hiyana ya macho na yanayoficha vifua))[3]
 
 
  1. Binaadamu hawezi kuficha kitu kwa Allaah, kwani ‘amali na siri zote zitadhihirika Siku ya Qiyaamah. [Aal-‘Imraan 3: 29, Az-Zumar 39: 7, Al-An’aam 6: 60, At-Tawbah: 94, Al-Jumu’ah 62: 8, Atw-Twaariq 86: 9].
 
  1. Ni muhimu kwa Muislamu kuzitekeleza amri za Dini yake na si kwa mandhari pekee. Na mara nyingi watu huwa ni wenye kusema pindi anapotenda jambo ovu kuwa: “Lakini niyyah yangu ni nzuri”. Hapa Muislamu anatakiwa aizingatie Hadiyth nyengine inayosema: ((Hakika Allaah Hatazami viwiliwili vyenu wala sura zenu, lakini Anatazama nyoyo na ‘amali zenu)).[4] Hivyo, ‘amali zinafaa ziende sambamba na Aliyoyateremsha Allaah na kuja nayo Mtume wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم).
 
  1. Usimhukumu mtu kwa mandhari yake, pindi ukimuona mtu shakili yake na hakuvaa mavazi ya Muumin ukadhania ni mtu muovu, huenda akawa ni mwema. Hali kadhalika, pindi ukimuona mtu shakili yake na mavazi yake ni ya ki-Muumin ukadhani kuwa ni mtu mwema kabisa, lakini huenda akawa ni mtu muovu.
 
  1. Kuzingatia yanayomridhisha Allaah (سبحانه وتعالى) daima.

Sababu 21 Za Kumfanya Muislam Asisherehekee Maulidi Nasiha Za Minasaba Mbalimbali




AlhamduliLLaah - Sifa njema zote Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Mola wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.
Zifuatazo ni sababu na hoja ambazo Muislam mwenye kupenda kufuata haki na mwenye kutaka apate uongofu ili abakie katika njia iliyonyooka na ajiepushe na mambo ya baatil. Hoja ni za wazi kutoka katika Qur-aan na Sunnah. Hoja za kupinga jambo hili ziko nyingi sana, lakini tulizozikusanya tunatumai kuwa zitamtosheleza Muislamu aikinaishe nafsi yake kuwa Maulidi ni jambo la uzushi katika dini kwa hiyo ni bora kutenda amali zile tulizopata mafundisho yake kutoka kwa Mtume صلى الله عليه وآله وسلم, Maswahaba wake na Salafus Swaalih (Watangu wema).

SABABU YA KWANZA:
Kumpenda Mola Mtukufu Aliyetuumba
Kwanza kabisa ni kwa sababu ya kumpenda Mola Mtukufu Aliyetuumba Ambaye Anataka kuhakikisha kuwa mapenzi yetu Kwake ni kumfuata Mtume صلى الله عليه وآله وسلم ambaye tokea kuzaliwa kwake hadi kufa kwake hakufanyiwa wala hakusherehekea siku yake ya kuzaliwa.

Anasema Allaah سبحانه وتعالى:
 ((قُلْ إِن كُنتُمْ تُحِبُّونَ اللّهَ فَاتَّبِعُونِي يُحْبِبْكُمُ اللّهُ وَيَغْفِرْ لَكُمْ ذُنُوبَكُمْ وَاللّهُ غَفُورٌ رَّحِيمٌ))
((Sema: Ikiwa nyinyi mnampenda Allaah basi nifuateni mimi, Allaah Atakupendeni na Atakufutieni madhambi yenu. Na Allaah ni Mwenye kufuta madhambi na Mwenye kurehemu)) [Al-'Imraan: 31]


SABABU YA PILI:
Kufuata amri yake Mtume صلى الله عليه وآله وسلم ya kushikamana na Sunnah Zake na Sunnah za Makhalifa wake
 (( أُوصِيكُمْ بِتَقْوى اللَّه، وَالسَّمْعِ وَالطَّاعَةِ وإِنْ تَأَمَّر عَلَيْكُمْ عَبْدٌ حبشيٌ ، وَأَنَّهُ مَنْ يَعِشْ مِنْكُمْ فَسَيرى اخْتِلافاً كثِيرا . فَعَلَيْكُمْ بسُنَّتي وَسُنَّةِ الْخُلُفَاءِ الرَّاشِدِينَ الْمَهْدِيِّينَ ، عضُّوا عَلَيْهَا بالنَّواجِذِ ، وإِيَّاكُمْ ومُحْدثَاتِ الأُمُورِ فَإِنَّ كُلَّ بِدْعَةٍ ضلالَةٌ )) رواه أبو داود ، والترمذِي وقال حديث حسن صحيح
((Nakuusieni kumcha Allaah, usikivu na twaa hata ikiwa kiongozi wenu (Au atakayekuamrishen) ni Mtumwa wa Habash. Mtakaoishi miongoni mwenu mtaona ikhtilafu nyingi. Kwa hiyo shikamaneni na Sunnah zangu na Sunnah za Makhalifa waliongoka baada yangu. Ziumeni kwa magego (zikamateni kwa nguvu wala msiziache). Na tahadharini na mambo ya uzushi kwani kila bid'ah ni upotofu)) [Abu Daawuud, At-Trimidhiy kasema Hadiyth Hasan Swahiyh]
Kwa hiyo inamtosheleza Muislamu hoja hii pekee ya kuwa Mtume صلى الله عليه وآله وسلم wala Maswahaba zake hawakusherehekea Maulidi, kumfanya naye asisherehekee.
Na hiyo ndio sababu kubwa ya Waislamu kukhitilafiana na kugawanyika makundi makundi. Amesema Imaam Maalik رحمه الله "'Hakuna kitakachotengeneza Ummah huu wa mwisho ila kwa kile kilichotengeneza Ummah wa mwanzo". Na maadam Salafus-Swaalih (watangu wema) hawakufanya bid'ah kama hii, sisi ni lazima tuwe na khofu kubwa ya kuifanya.


SABABU YA TATU:
Ametuamrisha Allaah سبحانه وتعالى tufuate aliyotuletea Mtume صلى الله عليه وآله وسلم na tujiepushe na aliyotukataza
 ((وَمَا آتَاكُمُ الرَّسُولُ فَخُذُوهُ وَمَا نَهَاكُمْ عَنْهُ فَانتَهُوا))
((Na anachokupeni Mtume chukueni, na anacho kukatazeni jiepusheni nacho)) [Al-Hashr: 7]


SABABU YA NNE:
Kufuata amri ya Kumtii Allaah سبحانه وتعالى na Mtume Wake صلى الله عليه وآله وسلم
Anasema Allaah سبحانه وتعالى katika Aayah nyingi kwenye Qur-aan:
((وَأَطِيعُوا اللَّهَ وَأَطِيعُوا الرَّسُولَ))
((Na mtiini Allaah na mtiini Mtume )) [At-Twaghaabun: 12]
Na kumtii Mtume صلى الله عليه وآله وسلم ni kumtii Allaah سبحانه وتعالى
((مَّنْ يُطِعِ الرَّسُولَ فَقَدْ أَطَاعَ اللّهَ))
((Mwenye kumtii Mtume basi ndio amemtii Allaah)) [An-Nisaa: 80]


SABABU YA TANO:
Kutokufuata amri ya Mtume صلى الله عليه وآله وسلم ni kumkhalifu na kupata adhabu kali
 ((فَلْيَحْذَرِ الَّذِينَ يُخَالِفُونَ عَنْ أَمْرِهِ أَن تُصِيبَهُمْ فِتْنَةٌ أَوْ يُصِيبَهُمْ عَذَابٌ أَلِيم))
((Basi nawatahadhari wanaokhalifu amri yake, usije ukawapata msiba au ikawapata adhabu chungu)) [An-Nuur: 63]


SABABU YA SITA:
Kumpinga Mtume صلى الله عليه وآله وسلم ni sababu ya kuingizwa motoni
 ((وَمَن يُشَاقِقِ الرَّسُولَ مِن بَعْدِ مَا تَبَيَّنَ لَهُ الْهُدَى وَيَتَّبِعْ غَيْرَ سَبِيلِ الْمُؤْمِنِينَ نُوَلِّهِ مَا تَوَلَّى وَنُصْلِهِ جَهَنَّمَ وَسَاءتْ مَصِيرًا))
((Na anayempinga Mtume baada ya kumdhihirikia uongofu, na akafuata njia isiyo kuwa ya Waumini, tutamuelekeza alikoelekea, na tutamuingiza katika Jahannamu. Na hayo ni marejeo maovu)) [An-Nisaa: 115]


SABABU YA SABA:
Kukhofu upotofu unaompeleka mtu motoni
Mtume صلى الله عليه وآله وسلم Alikuwa akitanguliza khutba zake kwa kutoa maonyo hayo:
(( إن خير الكلام كلام الله وخير الهدي هدي محمد صلى الله علي وسلم وشر الأمور محدثاتها وكل محدثة بدعة وكل بدعة ضلالة وكل ضلالة في النار)) أخرجه مسلم في صحيحه
((Maneno bora ni kitabu cha Allaah (Qur-aan) na Uongofu mbora kabisa ni uongofu wa Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم na jambo la shari kabisa ni uzushi, na kila jambo jipya (katika dini) ni bid'ah (uzushi) na kila bid'ah ni motoni)) [Muslim katika Swahiyh yake]


SABABU YA NANE:
Khofu ya kuwa miongoni mwa kundi litakaloingia motoni
Mtume صلى الله عليه وآله وسلم alipoonya katika Hadiyth ifuatayo kuwa makundi yote yanayojiita ni ya Kiislam na hali hayafuati mafunzo kama aliyokuja nayo yeye, yatakuwa motoni isipokuwa kundi moja. Maswahaba walishtuka na wakataka kujua ni kundi gani hilo moja, akawajibu kuwa ni kundi ambalo watu wake watakuwa wanafuata mwendo wake na wa Maswahaba zake.
((افترقت اليهود على إحدى وسبعين فرقة، وافترقت النصارى على اثنتين وسبعين فرقة، وستفترق هذه الأمة على ثلاث وسبعين فرقة كلها في النار إلا واحدة،)) فقال الصحابة: من هي يا رسول الله؟ قال: ((من كان على مثل ما أنا عليه وأصحابي)) الترمذي و الحاكم
((Waligawanyika Mayahudi katika makundi sabini na moja, na waligawanyika Manaswara katika makundi sabini na mbili, na utagawanyika Umma wangu katika makundi sabini na tatu, yote yataingia motoni ila moja!)) Maswahaba wakasema: 'Ni kundi lipi hilo Ee Mtume wa Allaah? Akajibu: ((Ni lile ambalo litakuwa katika mwenendo wangu hii leo na Maswahaba zangu)) [Imepokewa na Maimaam At-Tirmidhiy na Al-Haakim]


SABABU YA TISA:
Kuitikia wasiya wa Allaah سبحانه وتعالى ili kubakia katika njia iliyonyooka
Anasema Allaah سبحانه وتعالى
 ((وَأَنَّ هَذَا صِرَاطِي مُسْتَقِيمًا فَاتَّبِعُوهُ وَلاَ تَتَّبِعُواْ السُّبُلَ فَتَفَرَّقَ بِكُمْ عَن سَبِيلِهِ ذَلِكُمْ وَصَّاكُم بِهِ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ))
((Na kwa hakika hii ndiyo Njia Yangu Iliyonyooka. Basi ifuateni, wala msifuate njia nyingine, zikakutengeni na Njia yake. Haya Amekuusieni ili mpate kumcha Mungu)) [Al-An'aam: 153]


SABABU YA KUMI:
Vitendo visivyokuwa vya Sunnah havipokelewi
 (( من عمل عملاً ليس عليه أمرنا فهو رد)) البخاري
((Atakayetenda kitendo kisichokuwa chetu (katika dini yetu) basi kitarudishwa)) [Al-Bukhaariy]
Hivyo mtu atapoteza muda wake, labda na gharama ya kutekeleza bid'ah hii na kumbe amali hii haina thamani yoyote mbele ya Allaah.


SABABU YA KUMI NA MOJA:
Maulidi yamezushwa karne ya nne (miaka mia nne) baada ya kufa Mtume صلى الله عليه وآله وسلم na watu wenye kufru
Walioanzisha Maulidi ni viongozi wa Faatwimiyyun huko Misr (hawa walikuwa ni Rawaafidh (Mashia) katika dhehebu la Ismailiyah [Makoja] walianza kusherehekea Maulidi ya ‘Aliy bin Abi Twaalib (Radhiya Allaahu ‘anhu), na Maulidi ya Hasan na Husayn (Radhiya Allaahu ‘anhuma), na Maulidi ya Faatwimah az-Zahraa (Radhiya Allaahu ‘anha), na Maulidi ya kiongozi wao aliye hai kwa wakati ule. Sasa kwa nini tuwafuate wao? Na kama alivyotujulisha Mtume صلى الله عليه وآله وسلم kwamba watu bora kabisa wa kuwafuata ni wa karne tatu pekee aliposema:
((خير القرون قرني ثم الذين يلونهم ثم الذين يلونهم)) متفق عليه
((Karne zilizo bora kabisa ni karne yangu, kisha inayofuatia kisha inayofuatiya)) [Al-Bukhaariy na Muslim]


SABABU YA KUMI NA MBILI:
Makafiri wanafurahi Waislamu wanapofanya Bid'ah kwani ni kuacha mafunzo sahihi ya dini na ni kuzifuta Sunnah za Mtume صلى الله عليه وآله وسلم
Napoleon Bonaparte alimpa Shaykh Al-Bakriy Riyaal mia nane za Ufaransa (inasemekana ni mia tatu kwenye sehemu zingine) ili arudishe bid'ah ya Maulidi naye akahudhuria mwenyewe Maulidi. Maana makafiri wanajua kuwa Waislam wanaposhughulishwa na vipumbazo kama hivyo, husahau matakwa yao ya msingi na muhimu.


SABABU YA KUMI NA TATU:
Baadhi ya maneno katika Maulidi yana kufru ya kumpandisha Mtume صلى الله عليه وآله وسلم cheo cha usawa na Allaah سبحانه وتعالى wakati yeye ametuonya tusifanye hivyo
 ((لا تطروني كما أطرت النصارى المسيح ابن مريم، إنما أنا عبد، فقولوا: عبد الله ورسوله)) متفق عليه
((Msinitukuze Kama Manaswara walivyomtukuza Masiyh mwana wa Maryam, hakika mimi na mja kwa hiyo semeni mja wa Allaah na Mjumbe Wake)) [Al-Bukhaariy na Muslim]


SABABU YA KUMI NA NNE:
Wanapoinuka kumswalia Mtume صلى الله عليه وآله وسلم wanaamini kwamba roho yake inahudhuria wakati huo
Hii ni fikra ovu kabisa, na pia yeye mwenyewe alikuwa hapendi kuinukiwa alipokuwa hai, vipi mtu anayempenda amfanyie jambo analolichukia wakati amekufa?
Siku moja Maswahaba walikuwa wamekaa msikitini pamoja na Abubakar رضي الله عنه ambaye alikuwa akisoma Qur-aan. 'Abdullah ibn Ubbay ibn Saluul, mnafiki mkubwa alikuja akaweka takia na mto wake akaketi. Alikuwa ni mwenye sura nzuri na mwenye lugha ya ufasaha. Alisema: "Ewe Abu Bakar, muulize Mtume صلى الله عليه وآله وسلم atuonyeshe alama ya utume wake kama walivyotuonyesha Watume wengine. Mfano, Muusa عليه السلام ametuletea Ubao (wa Tauraat), 'Iysa عليه السلام alituletea Injiyl na meza ya chakula kutoka mbinguni, Daawuud عليه السلام alituletea Zabuur, Swaalih عليه السلام alitulietea ngamia wa kike" Abu Bakar رضي الله عنه aliposikia akaanza kulia. Mara akaingia Mtume صلى الله عليه وآله وسلم na Abu Bakar رضي الله عنه akawaambia Maswahaba wengine wainuke kumpa heshima Mtume صلى الله عليه وآله وسلم na kumpa malalamiko ya mnafiki. Mtume صلى الله عليه وآله وسلم akasema: ((Sikizeni! Msiniinukie mimi bali….
وَقُومُواْ لِلّهِ قَانِتِينَ
((na simameni kwa ajili ya Allaah)) [Al-Baqarah: 238] (dalili kutoka Tafsiyr Ibnu Kathiyr]


SABABU YA KUMI NA TANO:
Kuchanganyika kwa wanawake na wanaume
Jambo ambalo limekatazwa katika dini na katika sherehe hii kumedhihirika sana hasa pande za nchi zetu za Afrika Mashariki. Na uovu huu unafikia hadi kuimba kwa pamoja na kuchezesha vichwa kama kwamba ni dansi fulani. Imefika hadi maulidi kuitwa ‘disco maulidi’


SABABU YA KUMI NA SITA:
Kuwaigiza Manaswara
Manaswara wanasherehekea siku ya kuzaliwa 'Iysa عليه السلام kama wanavyodai. Na Waislamu haitupasi kusherehekea siku ya kuzaliwa Mtume صلى الله عليه وآله وسلم kwani tumefundishwa kuwa tufanye kinyume na wao katika mambo yetu.
Vilevile Mtume صلى الله عليه وآله وسلم kasema:
 ((خالفوا المشركين، أحفوا الشوارب، وأوفوا اللحى)) البخاري و مسلم
((Kuweni kinyume na Washirikina, punguzeni masharubu na fugeni ndevu)) [Al-Bukhaariy na Muslim]
Na kufanya hivyo (kusherehekea Maulidi) tutakuwa tunajifananiza nao, na jambo hilo la kuwaiga na kujifananisha na mambo yao limekatazwa kama alivyosema Mtume صلى الله عليه وآله وسلم:
 ((من تشبه بقوم فهو منهم )) أحمد و أبو داود
Anayejishabihisha na watu basi naye ni miongoni mwao)) [Ahmad, Abu Daawuud]


SABABU YA KUMI NA SABA:
Dini imekamilika hakuna tena haja ya kuleta mambo ya dini mapya
Kuzusha mambo mapya ya dini ni kama kumtuhumu Mtume صلى الله عليه وآله وسلم kuwa ametukhini mafunzo ya dini na hakuyakamilisha, bali kuna aliyoyaficha na hakutupa yote!! Na hali aliikamilisha dini kama ilivyompasa. Aayah hii chini iliteremshwa kudhihirisha ukamilifu wa dini ya Mola Mtukufu
 ((الْيَوْمَ أَكْمَلْتُ لَكُمْ دِينَكُمْ وَأَتْمَمْتُ عَلَيْكُمْ نِعْمَتِي وَرَضِيتُ لَكُمُ الإِسْلاَمَ دِينً))
((Leo Nimekukamilishieni Dini yenu, na nimekutimizieni Neema Yangu, na Nimekupendeleeni UISLAMU uwe ndiyo Dini)) [Al-Maaidah: 3]
Sasa vipi watu walete mafundisho ya dini mapya yasiyotokana na mafunzo kutoka kwa Allaah سبحانه وتعالى na Mtume Wake صلى الله عليه وآله وسلم ? Anauliza Allaah سبحانه وتعالى :
((أَمْ لَهُمْ شُرَكَاء شَرَعُوا لَهُم مِّنَ الدِّينِ مَا لَمْ يَأْذَن بِهِ اللَّهُ))
((Au hao wana miungu ya kishirikina waliowatungia dini asiyoitolea idhini Allaah?)) [Ash-Shuura 21]


SABABU YA KUMI NA NANE:
Kudhihirisha iymaan kwa kupenda yale aliyokuja nayo Mtume صلى الله عليه وآله وسلم pekee
عَنْ أَبِي مُحَمَّدٍ عَبْدِ اللَّهِ بِنْ عَمْرُو بِنْ العَاصِ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ : قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وآله وسلم: ((لا يُؤْمِنُ أَحَدُكُمْ حَتَّى يَكُونَ هَوَاهُ تَبَعَاً لِمَا جِئْتُ بِهِ )) حَدِيثٌ حَسَنٌ صَحِيحٌ، رَوَيْنَاهُ فِي كِتَابِ "الْحُجَّةِ بِإِسْنَادٍ صَحِيحٍ.
Kutoka kwa Abu Muhammad Abdullah Ibn 'Amr Bin Al-'Aasw رضي الله عنه ambaye alisema: Mtume صلى الله عليه وسلم kasema: ((Hatokuwa kaamini (kikwelikweli) mmoja wenu mpaka mapenzi yake yatakapomili (yatakapotii au kuwafikiana) kwenye yale niliyoyaleta)) (mafundisho) [Hadiyth Hasan iliyotoka katika kitabu “Al-Hujjah” ikiwa na mtiriko mzuri wa mapokezi].


SABABU YA KUMI NA TISA:
Kuacha mambo yenye shaka na kubakia katika yaliyo wazi
 عَنْ أَبي مُحمَّدٍ الحسَنِ بْنِ عليّ بْنِ أبي طَالِب، سِبْطِ رَسُولِ اللهِ صلى الله عليه وسلم وَرَيْحَانَتِهِ رضيَ اللهُ عنهُما، قالَ: حَفِظْتُ مِنْ رَسُولِ الله صلى الله عليه وسلم: ((دَعْ ما يَرِيبُكَ إلى مَا لاَ يَرِيُبكَ )) رَوَاهُ التِّرْمِذِيُّ وَالنَّسَائِيُّ وَقَالَ التِّرْمِذِيُّ: حَدِيثٌ حَسَنٌ صَحِيحٌ.
Kutoka kwa Abu Muhammad Al-Hasan Ibn ‘Aliy Ibn Abi Twaalib mjukuu wa Mtume صلى الله عليه وسلم na kipenzi chake رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمَا alisema: "Nilihifadhi kutoka kwa Mtume صلى الله عليه وسلم maneno haya: ((Acha kile kinachokutia shaka ufuate kile kisichokutia shaka)). [Imesimuliwa na At-Tirmidhiy na An-Nasaaiy, At-Tirmidhiy akisema kuwa ni hadiyth Hasan na Swahiyh].


SABABU YA ISHIRINI:
Mwezi huu wa Rabiy'ul Awwal ni mwezi alioaga dunia Mtume صلى الله عليه وآله وسلم , sasa vipi Muislamu asherehekee?
Wanachuoni wote wameafikiana kuwa siku hii ya tarehe 12 Rabiy‘ul Awwal ni siku aliyofariki Mtume صلى الله عليه وآله وسلم Vipi sasa watu watakuwa wanafurahi kwa siku kama hiyo? Anas bin Maalik رضي الله عنه anatuhadithia kuwa: "Hakuna siku ambayo watu wa Madiynah walikuwa na furaha ya hali ya juu kama siku aliyohamia Mtume صلى الله عليه وآله وسلم katika mji huo. Na hakuna siku ya huzuni kabisa kwa watu wa Madiynah kama siku aliyoaga dunia Mtume صلى الله عليه وآله وسلم ."
Inaonekana kama sisi tunakwenda kinyume na maadili ya wale watu bora waliokuwa wakimpenda Mtume صلى الله عليه وآله وسلم hata kuliko nafsi zao wenyewe.


SABABU YA ISHIRINI NA MOJA:
Sababu za Waislamu wanaoshikilia Bid'ah

1- Kufuata bila ya kupata elimu sahihi
Ukitaka kujua hoja za Waislamu wanaofuata bid'ah, hutopata kutoka kwao hoja nyingi kutoka katika Qur-aan na Sunnah, bali ni hoja za kutokana na rai zao tu, au watakwambia, 'kwani kuna ubaya gani?'. Na hata wakitoa hoja kutoka katika Qur-aan na Sunnah basi utakuta kwamba wanazifasiri dalili hizo isivyokusudiwa bali wanazishabihisha na matamanio yao kama Anavyosema Allaah سبحانه وتعالى :
((هُوَ الَّذِيَ أَنزَلَ عَلَيْكَ الْكِتَابَ مِنْهُ آيَاتٌ مُّحْكَمَاتٌ هُنَّ أُمُّ الْكِتَابِ وَأُخَرُ مُتَشَابِهَاتٌ فَأَمَّا الَّذِينَ في قُلُوبِهِمْ زَيْغٌ فَيَتَّبِعُونَ مَا تَشَابَهَ مِنْهُ ابْتِغَاء الْفِتْنَةِ وَابْتِغَاء تَأْوِيلِه))
 ((Yeye Ndiye Aliyekuteremshia Kitabu (hiki Qur-aan). Ndani yake zimo aayah Muhkam (nyepesi kufahamika) ambazo ndizo msingi (asili) wa Kitabu (hiki). Na ziko nyingine Mutashaabihaat (zinababaisha kama habari ya Akhera, za Peponi na Motoni na mengineyo ambao yamekhusika na Roho). Wale ambao nyoyoni mwao mna upotofu wanafuata zile zinazobabaisha kwa kutaka kuwaharibu watu na kutaka kujua hakika yake vipi)) [Al-'Imraan: 7]
Na ukizingatia utaona kuwa Waislamu wanaofuata Bid'ah sio wenye elimu kubwa ya juu, kwani ukilinganisha na wanaofuata Sunnah utaona kuwa kuna tofauti kubwa sana. Na hivyo ndivyo Allaah سبحانه وتعالى Anavyomjaalia kumpa elimu ya upeo wa juu yule mwenye kufuata haki. Na tujiulize Maulamaa wangapi wacha Mungu wenye elimu madhubuti wanafuata Bid'ah? Si rahisi kuwapata, bali ukiuliza wanaofuata Sunnah na wenye elimu kubwa ambayo athari yake tunaiona leo hii na itaendelea kizazi hadi kizazi InshaAllaah, utakuta ni wengi sana, miongoni mwao ni Maimamu wanne; Imaam Shaafi'iy, Ahmad bin Hanbali, Abu Haniyfah, Maalik, Sufyaan Ath-Thawry. Wasimulizi wa Hadiyth kina Al-Bukhaariy, Muslim, Abu Daawuud, At-Tirmidhiy, An-Nasaaiy, Ibn Maajah na kadhalika. Maulamaa maarufu; Ibn Taymiyah, ibnul Qayyim, ibnul Jawzy, ibnul Mubaarak, ibnu Hajar, ibnu Kathiyr, Imaam An-Nawawy, na waliopita katika miaka ya karibuni kama kina: ibn 'Uthaymiyn, ibn Baaz, Shaykh Al-Albaaniy na kadhalika. Hata katika jamii yetu kuna waliokuwa wamejaaliwa kupewa kipaji cha elimu kama kina Shaykh 'Abdullah Swaalih Al-Faarisy na kina Al Amiyn na Muhammad Qaasim Mazrui, Haarith Swaalih na wengineo wengi, bila kuwataja walio hai ambao hawana idadi kwa wingi wao.

2- Kufuata matamanio ya nafsi
Hufuata matamanio ya nafsi inavyopenda na sio kufuata haki. Wengine kutokana na unasaba wao huwa ni kwao kama utukufu kuwa nao wamo katika unasaba wa Mtume صلى الله عليه وآله وسلم
Anasema Allaah سبحانه وتعالى:
((وَلاَ تَتَّبِعِ الْهَوَى فَيُضِلَّكَ عَن سَبِيلِ اللَّهِ))
((Wala usifuate matamanio yakakupoteza kwenye Njia ya Allaah)) [Swaad: 26]

3- Ugumu wa kuacha mila uliotokana na mababa na mababu
Mitume waliopita walikuwa wakiwaita watu wao wawafuate waliyokuja nayo ya haki walipendelea kubakia katika ujinga na mila za mababa zao. Na Waislamu wenye kufuata mambo ya bid'ah nao ni vile vile ukiwauliza kwa nini hamuachi mambo yasiyo katika mafundisho ya Mtume صلى الله عليه وآله وسلم wanajibu hivyo hivyo kuwa 'vipi tuache Maulidi na hali tumekulia nayo?, au tutaachaje kitu ambacho mababa zetu walikuwa wakifanya?? Ina maana wao walikuwa hawajui?"
Anasema Allaah سبحانه وتعالى:
((وَإِذَا قِيلَ لَهُمْ تَعَالَوْاْ إِلَى مَا أَنزَلَ اللّهُ وَإِلَى الرَّسُولِ قَالُواْ حَسْبُنَا مَا وَجَدْنَا عَلَيْهِ آبَاءنَا أَوَلَوْ كَانَ آبَاؤُهُمْ لاَ يَعْلَمُونَ شَيْئًا وَلاَ يَهْتَدُون))
((Na wanapoambiwa: Njooni kwenye yale Aliyoyateremsha Allaah, na kwa Mtume, husema: Yanatutosha tuliyowakuta nayo baba zetu. Je, hata ikiwa baba zao walikuwa hawajui kitu wala hawakuongoka?)) [Al-Maaidah: 104]
Au walikuwa wakisema:
((بَلْ قَالُوا إِنَّا وَجَدْنَا آبَاءنَا عَلَى أُمَّةٍ وَإِنَّا عَلَى آثَارِهِم مُّهْتَدُونَ))
((Bali wanasema: Hakika sisi tuliwakuta baba zetu wanashika dini makhsusi, basi na sisi tunafuata nyayo zao)) [Az-Zukhruf: 22]

4- Kukhofu kutokuungana na wengi wanaofuata bid'ah
Wengine ukiwauliza kwa nini unafuata bid'ah ya Maulidi. Jibu ni kuwa anakhofu kuwa yeye peke yake ataonekana kuwa hasomi Maulidi katika kundi lake, na hii ni hatari ya kukhofu watu badala ya kumkhofu Mola Mtukufu na pia ni kwenda na mkumbo kwa kudhani kuwa wengi ndiyo wenye haki! Haya Anatueleza Allaah kuwa:
((وَإِن تُطِعْ أَكْثَرَ مَن فِي الأَرْضِ يُضِلُّوكَ عَن سَبِيلِ اللّهِ إِن يَتَّبِعُونَ إِلاَّ الظَّنَّ وَإِنْ هُمْ إِلاَّ يَخْرُصُونَ))
((Na ukiwatii wengi katika hawa waliomo duniani watakupoteza na Njia ya Allaah. Hawa hawafuati ila dhana tu, na hawakuwa ila ni wenye kusema uwongo tu)) [Al-An'aam: 116]

5- Wengine wanasema kuwa ni kudhihirisha mapenzi ya Mtume صلى الله عليه وآله وسلم
Je, mapenzi ya Mtume صلى الله عليه وآله وسلم yadhihirike siku moja tu? Au katika mwezi huu tu? Na si siku zote? Hayo bila shaka ni mapenzi ya uongo. Mapenzi ya kweli ni yale ya kumkumbuka siku zote na kumtii umpendaye. Haya ya Maulidi hayana moja kati ya mawili hayo.
6- Hoja ya kusema ni Bid'atun-hasanah (uzushi mzuri)
Mojawapo yao ni kuwa Maulidi ni Bid'atun-hasanah. Katika dini ya Kiislamu hakuna bid'ah nzuri kwani Mtume صلى الله عليه وآله وسلم alipotuonya alisema 'Kullu Bid'atin Dhwaalaah' (kila bid'ah ni upotofu). Na ikiwa kauli hii wanaipinga kuwa sio KILA bid'ah, basi wanasemaje kuhusu kauli ya Allaah سبحانه وتعالى Anaposema:
 ((كُلُّ نَفْسٍ ذَآئِقَةُ الْمَوْتِ))
((Kila nafsi itaonja mauti)) [Al-'Imraan: 185]
Je, tupinge pia kauli hii kuwa sio KILA nafsi? Na je, ina maana kuwa kuna watu wengine watabakia hawatokufa na hali tunatambua kuwa hakuna atakayebakia ila Mwenyewe Mola Mtukufu?
Tunamuomba Allaah سبحانه وتعالى Atuhidi kwa kutuonyesha yaliyo haki ili tuyafuate na Atuonyeshe yaliyo baatil tujiepushe nayo. Aamiyn.